Habari kutoka na

Lugha za Pili Zinazoongozwa Kuzungumzwa Zaidi Afrika

Don Osborne anajadili habari iliyowekwa kwenye tovuti ya Chuo Kikuu cha Olivet Nazarene ikionesha ramani ya “Lugha za pili kuzungumzwa zaidi duniani.” Anaeleza matatizo makuu kutokana na habari hiyo: Suala la kwanza ni kudhani kwamba “lugha inayozungumzwa zaidi kwenye nchi yoyote huwa wazi; mara nyingi, ni lugha ya taifa husika.”...

Maneno Yasiyotafsirika Yafafanuliwa kwa Michoro

  1 Juni 2014

Tovuti ya Pijamasurf [es] inazungumzia “orodha ya maneno 30 yasiyotafsirika” ambayo msanii mchunguzi Anjana Iyer [en] alijaribu kuyachorea mchoro wenye kuchekesha kidogo. Kwa mfano: Bakku- shan (Kijapani) Msichana mzuri…almuradi tu anaangaliwa kutokea nyuma. Unaweza kuipata orodha hiyo hapa.

Honduras Yazindua Kamusi ya Mtandaoni ya Lugha za Asili

  28 Februari 2014

Kamusi ya lugha za asili nchini Honduras ilisambazwa mtandaoni hivi karibuni[es]. Gazeti la Honduras liitwalo Tiempo [es] linaeleza kuwa kamusi hii “imejumuisha maneno yanayofanana katika lugha ya Kihispaniola, chortí, garífuna, isleño, miskito, pech, tawahka na tolupán, lugha ambazo ndizo zinazotengeneza urithi wa lugha wa nchi hiyo.”  Kwa mfano, unapotafuta neno...

Wikipedia kwa Lugha ya Ki-Guarani

  2 Novemba 2013

Mwaka huu, Wikipedia katika lugha ya Kihispaniola ilifikia makala milioni moja na kutolewa kwa mwongozo msingi wa mtumiaji katika lugha ya ki-Guarani. Wazo ni kufufua jamii ya wanaozungumza kiguarani katika jukwaa hili kubwa. Hadi sasa kuna makala 20 tu katika lugha hiyo. […] Kama una nia ya kushirikiana na mradi...

Alfabeti Hufurahisha na Kuhuzunisha Nchini Bulgaria

[…] Mojawapo ya likizo safi na takatifu zaidi nchini Bulgaria! Ni sherehe itupayo fahari ya kuwa tumetoa kitu chochote duniani! Ni likizo isiyohusiana na waasi wowote, vita, wala vurugu, ingawa hutujaza uzalendo na furaha. […] Unapotembea katika mitaa, mabango ya ugenini na maelekezo, yanazidi haya tuliyonayo kwetu kwa mbali sana...

Msumbiji: Je, ni Lugha Ngapi Zinazungumzwa Nchini?

Kuna lugha 20 zinazozungumzwa nchini Msumbiji, kwa mujibu wa tovuti ya serikali, zaidi ya lugha ya serikali ya Kireno. Carlos Serra [pt] anajiuliza kama kuna lugha nyingine zaidi, kwa mujibu wa wataalamu wa lugha mashuhuri:”Kuna mtu aliniambia kuwa zipo kati ya 20 na 26; mwingine akaniambia zipo 17 zilizoandikwa na...

Karibea: Tuzo za Fasihi ya Kifaransa

Wiki hii, waandishi wawili wenye asili ya Kiafrika wanaoandika kwa Kifaransa walipewa tuzo mbili zenye kuheshimika sana katika fasihi ya Kifaransa: Ulimwengu wa blogu za wanaozungumza Kifaransa katika Karibea umekuwa ukinguruma juu ya kutosheka kwao mara mbili kwa mpigo, katika makala hii kutoka Haiti, na hii kutoka Guadeloupe na hii...