Habari kutoka na

Twiti ya kwanza kutoka kwa Rais wa Madagaska

Rais mteule wa Madagaska Hery Rajaonarimampianina amefungua akaunti yake ya mtandao wa twita mnamo tarehe 23 Machi, 2014. Hii ndiyo twiti yake ya kwanza :  Kuna uwezekano mkubwa kuwa hiyo ndiyo twiti maarufu kutoka kwa mkuu wa nchi. Ni Rupert Murdoch anaweza kuwa na wasiwasi na kiwango cha “ukubwa/umaarufu” wa...

China: Jukumu la Baba

  2 Disemba 2013

Mtandao wa Offbeat China umeanzisha kipindi kipya na maarufu cha televisheni kinachojulikana kwa jina la “Baba, tunaelekea wapi?”. Kipindi hicho kinawakutanisha akina baba watano maarufu pamoja na watoto wao kwa ajili ya kufanya kazi mbalimbali za nje kwa lengo la kushindana na bila ya uwepo wa wake zao. Hapa chini,...

Udadisi wa Sami Anan

Mwanablogu wa Misri Zeinobia anatoa maoni yake machache kuhusu kuibuka tena kwa Sami Anan, Mnadhimu mkuu wa zamani wa Majeshi ya Misri. Je, ana mpango wa kugombea urais? Mwanahabari wa Sauti za Dunia Mtandaoni Victor Salama anasimulia zaidi.

Mwandamanaji Amtaka Morsi Kuondoka Kwa Lugha ya Mafumbo

Maandamano makubwa ya kumtaka rais wa Misri Mohamed Morsi ajiuzulu yanaendelea nchini Misri kwa siku ya tatu sasa. Kwenye mtandao wa Twita, Assem Memon anaweka picha iliyopigwa kwenye maandamano: @AssemMemon: Bango la Maandamano. Neno ondoka limeandikwa katika lugha 14 za mafumbo. Picha imewekwa kwenye mtandao wa Twita na @ alaafareed pic.twitter.com/S7OOSDfpV6

Kitabu kipya cha michezo ya watoto kutoka nchi mbalimbali

  7 Juni 2012

Blogu changamfu la Kimataifa, PocketCultures limechapisha limechapisha kitabu kuhusu michezo kumi na tano ya watoto kutoka nchi mbalimbali na amabayo inaweza kuchezwa kwa urahisi na msomaji. Kitabu kinaitwa ‘Games for Kids of the World’ na kinaweza kupatikana kwa bure kwenye iPad, Mac au kwenye kompyuta.