Habari kutoka Muhtasari wa Habari na Haki za Mashoga
Kuhusu Kuwa Kijana, Mweusi na Mgeni nchini Afrika Kusini
Leila Dee Dougan anaweka video ya muziki inayotoka kwenye toleo la hivi karibuni la msanii wa Afrika Kusini Umlilo: Umlilo (ambaye hapo awali aliandikwa kwenye tovuti ya Africa is a Country) anaendelea kupunguza mipaka ya kijamii, akivunja vunja mila zinazohusu masuala ya jinsia na mapenzi kwa kutumia albamu yake ya...
Uchambuzi zaidi Kuhusu Muswada wa Kupinga Ushoga Nchini Uganda
Kristoff Titeca anaangalia mbali zaidi ya sababu moja kuhusiana na muswada wa kupinga ushoga nchini Uganda: Pointi muhimu ni kuwa Rais Museveni hajawahi kuwa shabiki mkubwa wa muswada huu na badala yake amekuwa mtu wa kuutilia mashaka: alikuwa anafahamu matokeo mabaya kimataifa. Katika majibu yake ya wazi kwa mara ya...
Taiwan: Maandamano Dhidi ya Sheria Juu ya Usawa Kwenye Ndoa
Wabunge wa Yuan nchini Taiwan walipitisha muswada wa kwanza ya “Usawa kwenye Ndoa“ [zh] mnamo Oktoba 25, 2013. Novemba 30, zaidi ya watu 300,000 walipinga muswada huu, hasa dhidi ya pendekezo juu ya ndoa za jinsia moja. J. Michael Cole, mwandishi wa habari wa kujitegemea mkaazi wa Taipei, alielezea kile...
Gwaride la Kwanza la Mashoga Nchini Lesotho
Leila Hall anablogu kuhusu gwaride la kwanza la mashoga kuwahi fanyika nchini Lesotho: Tukio hilo limeandaliwa na Kikundi cha Kutoa msaada cha MATRIX- Shirika lisilo la kiserikali la Lesotho- linatetea haki za watu kama wasagaji, mashoga, wenye hisia za mapenzi kwa jinsia zote mbili, Wanaogeuza jinsia nchini humo. Shirika hilo, ambalo lilitambuliwa kisheria mwaka...
Mashoga Washambuliwa Kaskazini mwa Kameruni
Oscarine Mbozo’a anaripoti [fr] katika blogu ya L'Actu kuwa shoga mmoja akiwa ameambatana na mwenzi wake walizomewa karibu na soko mnamo tarehe 6, Januari 2013, mjini Maroua, Kaskazini mwa Kameruni: Goche Lamine, mfanyabiashara wa madawa, alikamatwa na mwanafunzi wa shule ya sekondari aitwaye Sanda, mwenye umri wa miaka 17. Umati wa...
Utambulisho wa Jamii ndogo ya Balkan
Waandishi vijana kumi na watano kutoka katika nchi zipatazo sita tofauti wametengeneza mfululizo wa masimulizi binafsi kuhusu masuala ya namna jamii zenye watu wachache (kwa mapana yake) zinavyoweza kuwakilishwa kutoka Bosnia na Herzegovina, Kosovo, Serbia, na Macedonia. Habari zinapatikana katika lugha za Kiingereza, Kijerumani, na Kifaransa katika mwonekano wa tovuti...