Habari kutoka Muhtasari wa Habari na Sanaa na Utamaduni
‘Escopetarra': Chombo cha Kipekee
Kama unaamini kuwa hakuna jambo zuri linaloweza kutokana na bunduki aina ya gobore, basi unapaswa kukifahamu kifaa kiitwacho “escopetarra”— mchanganyiko uliotokana na kubadilisha silaha mbili “hatari” (an AK-47 na gitaa) na kuwa kifaaa cha amani. “Escopetarra” ni neno lililotokana na muunganiko wa maneno ya Kispaniola, “escopeta” (bunduki) na “guitarra” (gitaa). Kwenye...
Wanawake Wanaovaa Nusu Uchi Wataiokoa Sekta ya Utalii Kenya?
Je, kutembea uchi yanaweza kuwa mbinu bora ya kufufua sekta ya utalii nchini Kenya kufuatia mashambulizi ya wanamgambo wa Al Shabaab?: Seneta mteule, Mbura anasemekana kuwaomba wanawake katika mkoa wa pwani kutembea nusu uchi ili kuwavutia watalii zaidi kuzuru eneo hilo. Wito huo umeibua maswali kuhusiana na thamani ya mwanamke...
Umoja wa Ulaya Hautatoa Nafuu ya Kodi ya VAT kwa Vitabu ya Kidigitali
Mnamo Machi 5, 2015, Mahakama ya Haki ya Umoja wa Ulaya ilitoa hukumu kwamba punguzo la kodi ya ongezeko la thamani (VAT) lililotolewa kwa vitabu vinavyochapishwa halitahusisha vitabu vya kidijitali, kwa kuzingatia kwamba kila kinachosambazwa au kutolewa kwa mfumo wa kieletroniki au kwa mtandao wa intaneti ni huduma. Amalia Lopez anahoji...
Wachoraji 10 wa Kiafrika wa Vitabu vya Watoto Unaopaswa Kuwajua
Jennifer Sefa-Boakye anasaili orodha ya washindani 10 bora zaidi wa tuzo ya Golden Baobab kwa Wachoraji wa Kiafrika: Mwaka jana shirika la Afrika lenye makazi yake nchini Ghana, Golden Baobab, liliwatambulisha wachoraji kadhaa wenye vipaji, ambao kazi zao ni kama vile masimulizi ya Ashanti yaliyosukwa kutoka miji ya Moroko na...
Tafakari ya Suala la Kuoa Nje ya Tabaka lako Nchini India
Karthik Shashidhar, mshauri huru wa utawala na mwanasayansi wa takwimu, anaonesha takwimu kutoka kwenye utafiti wa kitaifa wa Afya ya Familia. Shashidhar anajadili idadi ya wanawake nchini India ambao wameolewa na watu wenye tabia lao wenyewe.Mfumo wa kimatabaka wa kihindi nchini India unaongozwa na amri ya makundi ya makundi ya kuoana...
Maktaba ya Digitali ya Tiba Asilia Nchini Ufilipino
Ikiwa imeanzishwa na mamlaka kadhaa za kiserikali, Maktaba Dijitali ya Elimu ya Tiba za Jadi Ufilipino (TKDL-Health) inalenga kuweka kumbukumbu na kufanya masuala ya tiba za jadi kuwa za kidijitali nchini humo. Jamii, ambazo nyingi ni zile za miliamni au majirani zao, zimekuwa zikitegemea miti na mazao mengine ya asili...
Ousmane Sow : Mwafrika Mweusi wa Kwanza Kushiriki katika Taasisi ya Kifaransa ya Sanaa
Mchonga sanamu Msenegali, Ousmane Sow, alikaribishwa kwenye Académie des Beaux-Arts de Paris [Taasisi ya Sanaa ya Paris] tarehe 11, mwezi wa Disemba. Africa-top-talents.com inaripoti kwamba: Une belle consécration pour ce sculpteur sénégalais connu pour ses séries de sculptures monumentales consacrées aux ethnies africaines (noubas, peuls, masaï, Zoulou). « Mon élection a d’autant plus de valeur à mes yeux...
Kutana na Joshua Beckford Aliyehudhuria Chuo Kikuu cha Oxford Akiwa na Umri wa Miaka 6
Blogu ya Omg Ghana iliripoti kuhusu mafanikio bora ya kielimu ya Joshua Beckford: Katika umri wa miaka 8, wewe pengine ulikuwa unafanya mazoezi ya michezo au ulikuwa ukifanya maandalizi ya kujiunga na daraja la tatu. Naam, kutana na Joshua Beckford mwenye umri wa miaka 8. Huyu yuko juu ya wastani wa...
Fasiri ya Lugha ya Kikannada ya Karne ya 11 Yapatikana kwenye Mfumo wa Wikisource
Vachana Sahitya ni aina ya uandishi kwa mtindo wa sauti katika lugha ya ki-Kannada ambao ulianzia karne ya 11 na kukua sana kwenye karne ya 12. Makala ya Subhashish Panigrahi inaripoti (ikiwa imeandikwa kwa ushirikiano wa Pavithra Hanchagaiah na Omshivaprakash) kwenye blogu ya Wikimedia kwamba waandishi wawili wa Wikimedia wakishirikiana...
Sinagogi Pekee Lililobaki Myanmar
Lilijengwa miaka 120 iliyopita, Sinagogi la Musmeah Yeshua lililoko eneo la Yangon ni Sinagogi pekee la wayahudi lililoyobaki katika eneo linaloongozwa na waumini wa dini ya Kibudha waishio nchini Myanmar. Mbali na kuwa kivutio cha utalii, pia limetajwa kama jengo la urithi la mambo ya kale katika mji huo.