Habari kuhusu Picha kutoka Aprili, 2014
Mashabiki Jijini Skopje Wakusanyika Kubadilishana ‘Stika’ za Soka
Mamia ya watu walikusanyika mchana wa Jumapili kwenye eneo la wazi jijini Skopje kubadilishana ‘stika’ za mkusanyiko rasmi wa picha za Kombe la Dunia la FIFA tarehe 28 Aprili, 2014. Nchini Macedonia, kama ilivyo kwa nchi nyinginezo za Yugoslavia ya zamani, utamaduni wa kukusanya ‘stika’ una historia ndefu, inaanzia miaka...
Mzazi wa Kisyria Auomba Ubalozi wa Uingereza Kumwunganisha na Mwanae
Wael Zain, raia wa Syria anayeishi Londona, ametumia mtandao wa Twita kutafuta kusikilizwa madai yake kuwa mwanae wa kiume mwenye uraia wa Uingereza ametelekezwa Syria kwa miaka mitatu sasa.
Gazeti la Kifaransa Lachapisha Chati Inayoonyesha Mataifa Yanayoongoza kwa Uhalifu
Gazeti la Le Progrès la jijini Lyon, Ufaransa ilichapisha chati [fr] yenye jina la “”Délinquance : à chacun sa spécialité – principales nationalités impliquées” (Uhalifu: Mataifa yanayohusishwa zaidi na [kila aina ya uhalifu]) (Ona picha katika mtandao wa twita hapa chini): Dans son édition du jour, Le Progrès ose publier un...
Serikali Mpya ya Waziri Mkuu Roger Kolo Yatangazwa Nchini Madagaska
Mtandao wa Tananews nchini Madagascar umechapisha orodha kamili ya mawaziri 31 wa serikali mpya ya Madagaska [fr]. Mitsangana Madagascar anasema kwamba orodha hiyo ina wanawake 6 na kuwa mawaziri 7 walikuwa kwenye baraza[fr] la serikali iliyopita ya mpito. Waziri mkuu wa zamani Beriziky aliitakia serikali kila la heri kwenye mtandao...
Niger Yapata Kituo Chake cha Kwanza cha Reli Baada ya Kusubiri kwa Miaka 80
Aprili 7, Niger ilizindua katika mji mkuu wa Niamey kituo chake cha kwanza cha treni kuwahi [fr]. Mamlaka tayari ilikuwa na makadirio ya ujenzi wa kituo cha treni miaka 80 iliyopita lakini mradi kamwe haukuanzishwa. Tukio hilo litaanzisha ujenzi wa reli kati ya Niger, Benin, Burkina Faso na Côte d'Ivoire....
PICHA: Maandamano mjini Caracas, Aprili 1
Tovuti ya PRODAVINCI inachapisha picha nne za Andrés Kerese zilizopigwa wakati wa maandamano yaliyotokea Chacao, moja ya mitaa ya wilaya ya Caracas, Jumanne, Aprili 1, 2014.
Jijini Havana Unapata Kitabu Bure, Bila Malipo
"Kitabu hiki kinamilikiw ana yeyote atakayekipata na kukitoa tena baada ya kukisoma ili watu wengine wakifurahie."
Hadithi ya Mapenzi Kibera
Hii ni hadithi ya kusisimua ya mapenzi kati ya Sam, anayetoka Kibera, makazi ya masikini kwenye jiji la Nairobi, Kenya, na Alissa, anayetoka Minnesota, Marekani: Bila shaka, hii ni hadithi ya mapenzi isiyo na kifani mwaka huu!!! Alissa anatoka Minnesota, huko Sam alizaliwa na kulelewa Kibera. Ilikuwaje ‘njiwa hawa wa...