Habari kuhusu Teknolojia kutoka Agosti, 2010
Mashindano ya Video: Intaneti Kama Chombo cha Kueneza Amani
Mfumo wa Intaneti umependekezwa kwa ajili ya kupata Tuzo ya Amani ya Nobel kwa mwaka 2010. Kama sehemu ya mjadala unaoendelea kuhusu mchango wa Intaneti katika jamii nzima ya binadamu , Condé Nast na Google Ireland wameungana na kuandaa mashindano haya ya video na mshindi atapata fursa ya kusafiri na pia video yao kuoneshwa kupitia MTV ya Italia.
Italia: HAPANA kwa Vikwazo Dhidi ya Uhuru wa Kujieleza wa Mtandaoni
Muswada mpya wa habari na Unasaji wa siri wa Mawasiliano ambao umewasilishwa kwenye bunge la Italia unaweza kuanzisha "hatari ya malipo ya fidia" kwa wanablogu wote na vyombo vya habari vya mtandaoni.