Habari kuhusu Teknolojia kutoka Machi, 2010
Siku ya Ada Lovelace: Kuwapongeza Wanawake Wanajishughulisha Kupigania Teknolojia na Uwazi Ulimwenguni
Katika kusherehekea Siku ya Ada Lovelace tunawaletea makala fupifupi kuhusu wanawake kadhaa walio sehemu mbalimbali duniani ambao hutumia teknolojia ili kuzifanya serikali ziwe wazi na zinazowajibika zaidi.
Global Pulse 2010: Mwaliko wa kuzungumza na watoa uamuzi mtandaoni
Kuanzia tarehe 29 hadi 31 Machi, vuguvugu linalojulikana kama Global Pulse 2010, yaani Mapigo ya Moyo ya Ulimwengu 2010, linakusudia kuwakusanya jumla ya watu 20,000 kupitia mtandao ili wafanya mazungumzo kuhusu mada mbalimbali kuanzia zinazohusu maendeleo ya binadamu hadi sayansi na teknolojia.
Ghana: tamasha la Twestival 2010 Mjini Accra: Shughuli Yenye Maana?
Kama uanahabari wa kijamii unabadilisha mtindo ya mawasiliano katika nchi za Magharibi, basi kwa hakika haujapungukiwa katika kufikia sehemu zinazovutia barani Afrika. . Kwa hiyo haishangazi kwamba MacJordan, wa Global Voices, anashirikiana na Rodney Quarcoo ili kulifikisha tukio hili la kuburudisha kwa watu wa Ghana.
Sudani: Je, Teknolojia ya Habari na Mawasiliano Itafanya Kazi?
Jarida la The Financial Times liliripoti hivi karibuni kuwa mpango wa mamilioni ya dola wa Benki ya Dunia wa kusambaza kompyuta na upatikanaji wa Intaneti huko Juba, mji mkuu wa Sudani ya Kusini, umeshindwa. habari hizi zinazua swali: kelele zinazoambatana na teknolojia ya Habari na Mawasiliano (ICT) zina uhalali?