Habari kuhusu Teknolojia kutoka Novemba, 2009
Palestina: Mtaa wa Twita
Eman katika AquaCool anatoa maoni kuhusu mtaa wa kwanza kupata jina linalotokana na huduma ya Twita, katika kambi ya wakambizi huko ukingo wa Magharibi.
Ofisa Aweka Wazi Ufisadi wa Polisi kupitia Mtandao
Mnamo tarehe 6 Novemba, afisa wa polisi katika Idara ya Mambo ya Ndani huko Novorossiysk alitumia tovuti yake binafsi kuwasiliana na Waziri Mkuu Vladimir Putin na kuzungumzia matatizo lukuki yanayowakabili maafisa wa polisi nchini Urusi.
Vijana wa Kiyahudi na Kipalestina Watumia Video Kuuelewa Mgogoro
Mashirika mawili tofauti nchini Israel na katika Majimbo ya Palestina yanatumia zana za video ili kuwasaidia vijana wa Kiarabu na Kiyahudi kuuelewa mgogoro na kujenga daraja kati yao.
Tunisia: Mwanablogu Fatma Arabicca Awekwa Kizuizini
Mwanablogu wa Kitunisia Fatma Riahi ambaye hublogu kama Fatma Arabicca, ameshtakiwa kwa udhalilishaji katika blogu yake na hivi sasa amewekwa kizuizini.Kundi limeundwa kwenye Facebook kumuunga mkono mwanablogu huyu mwenye umri...
Kutambulisha Sauti Zinazotishwa
Leo, kitengo cha utetezi cha Global Voices, kinazindua tovuti mpya inayoitwa Threatened Voices, yaani, Sauti Zinazotishwa ili kusaidia kufuatilia unyamazishaji wa uhuru wa kujieleza wa mtandaoni. Inaonyesha ramani ya dunia na mwingiliano wa saa unaosaidia kuonyesha taarifa za vitisho na ukamataji unaofanywa dhidi ya wanablogu duniani kote, na ni mhimili mkuu wa kukusanyia taarifa kutoka katika asasi na wanaharakati walioamua kujitoa muhanga kwelikweli.
Tamasha la Blogu Indonesia
Tulitembelea tamasha la blogu la Indonesia au PestaBlogger 2009. Hii nim ara ya tatu kwa tukio hili la mwaka kufanyika. Tukio hili lilishuhudia wanablogu kutoka kila sehemu ya Kisiwa hiki ambacho pia ni Taifa wakimiminika mjini Jakarta ili kusherehekea, kujadili na kujumuika.
Kenya: Ramani Mpya Ya Wazi ya Kitongoji Cha Kibera Kwenye Blogu
Mradi wenye lengo la kutengeneza ramani mpya ya wazi ya kitongoji cha Kibera mjini Nairobi, Kenya: “Na jana tulimaliza siku nzima pale MS Action Aid kenya, ambako wanafunzi wa ki-Denmark...
Saudia Arabia: Ambako Kuiga Kazi Kinyume cha Haki Miliki ni Kosa la Jinai
Wanablogu wa Kisaudia wanaungana ili kumuunga mkono mwanablogu mwenzao anayelituhumu gazeti moja kuwa limetumia picha na kuzinakili kutoka mwenye blogu yake bila ruhusa.