Habari kuhusu Teknolojia kutoka Februari, 2009
Dunia Nzima: Lugha 2,500 Zinapotea
Ramani shirikishi ya lugha zinazopotea, inayoonyesha lugha 2,500 kati ya 6,000 ambazo ziko hatarini, imezinduliwa na Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa (UNESCO). Shirika hilo la kimataifa linawaomba watumiaji wachangie kwa kutuma maoni kwenye mradi huo ambao unawatia mashaka wanablogu wengi wenye nia ya kuhifadhi tamaduni.
Malawi: Homa Ya Uchaguzi na Kuelea Teknolojia ya Kidijitali
Juma lililopita lilikuwa lenye moto wa kisiasa kwa Wamalawi wengi kwani wameshuhudia wagombea wa viti vya urais na ubunge wakiwasilisha maombi yao kwenye Tume ya Uchaguzi kuelekea Uchaguzi utakaofanyika terehe 19 Mei. Hadi kufikia mwisho wa zoezi hilo wagombea wapatao 10 waliwasilisha maombi yao ya kugombea urais na mamia wengine kwa ajili ya kugombea viti 193 vya bunge.
Kampuchea: Vikwazo Vya Intaneti Vyalenga Wasanii
Wizara ya Masuala ya Wanawake nchini Kampuchea imetishia kuizuia tovuti yenye michoro ya wacheza ngoma ya Apsara walio vifua wazi pamoja na mwanajeshi wa Khmer Rouge. Uchujwaji wa habari wa namna hii unawalenga wasanii wanaotambulika zaidi kwa uwepo wao katika mtandao wa intaneti.
Bahrain: Mabloga Waungana Kupinga Uamuzi wa Kufungwa Kwa Tovuti
Wanablogu wa Bahrain wameujia juu uamuzi wa Waziri wa Habari wa nchi hiyo wa kuzuia upatikanaji wa tovuti mbalimbali, kadhalika kuzuia matumizi ya tovuti vivuli [proxy sites] zinazoruhusu watumiaji kuperuzi tovuti nyingine zilizozuiwa na zana za kuchuja habari. Ayesha Saldanha anaangalia maoni kutoka Bahrain.