Habari kuhusu Teknolojia kutoka Januari, 2009
Blogu za Afrika Zapendekezwa Kupokea Tuzo ya Bloggies 2009
Blogu zilizopendekezwa kwa ajili ya Tuzo ya Tisa ya Zawadi za Weblog: Mapendekezo ya blogu katika mashindano ya Bloggies ya 2009 yalifunguliwa tarehe 1 Januari na kufungwa tarehe 19 Januari. Kwa mujibu wa waandalizi, mashindano hayo ya Bloggies ni mashindano ambayo yamedumu kwa muda mrefu zaidi mtandaoni, na mapendekezo pamoja na uchaguaji wa washindani katika fainali, ni juu ya msomaji wa blogu. Mshindi hupata senti 2,009 za Marekani! Je, ni mabloga gani wa Kiafrika waliopendekezwa kwa ajili ya kinyang'anyiro cha blogu bora zaidi?
Palestina: Mawasiliano na Gaza
Katika mazingira ya kawaida bila kiwango kikubwa cha wanaojua kusoma, usambaaji wa intaneti husimama kati ya asilimia 13 mpka asilimia 15 (Gaza na Ukingo wa Magharibi kwa pamoja). Kutokana na mashambulizi yanayoendelea huko huko Gaza, uwezo wa kutumia intaneti umepungua sana. Japokuwa kuna idadi ndogo ya wanablogu wanaoandika moja kwa moja kutokea Gaza, wakazi wengine wengi wanatumia ujumbe wa maandishi wa simu za mkononi pamoja na simu nje ya nchi katika matumaini kwamba ushahidi wao utapata sehemu ya kuelezwa.