Habari kuhusu Michezo

Peru: Mchezaji wa Kandanda Afariki Dunia Uwanjani

  22 Julai 2013

Dakika tano kabla ya kumalizika kwa mchezo kati ya timu zaReal Garcilaso na Sporting Cristal, mchezaji nyota wa timu ya Sporting Cristal mwenye miaka 18 Yair José Clavijo alipata mshituko wa moyo na akapoteza maisha. Madaktari wa timu hiyo walijaribu bila mafanikio kunusuru hali yake akiwa kwenye sehemu ya kuchezea...

Uganda: Kukumbuka milipuko ya mabomu ya 2010

Wananchi wa Uganda wameutumia mtandao wa Twita na Facebook kuwakumbuka wahanga 2010 wa milipuko yha mabomu iliyotokea kwenye klabu ya Rugby huko Kyaddondo na katika baa ya Kijiji cha Kiethiopia jijini Kampala Uganda.Mashambulizi hayo yalitokea wakati ambao wapenzi wa kandanda walikuwa wakitazama mpambano wa fainali kati ya Uhispania na Uholanzi uliofanyika nchini Afrika Kusini.

Paralympiki 2012: Mwanzo mzuri, Habari za Kukumbukwa

  16 Septemba 2012

Martine Wright, aliyenusurika mlipuko wa mabomu uliotokea London, Rim Ju Song, mshiriki wa kwanza kutokea Korea Kaskazini ambaye, miezi michache iliyipita, hakuweza kuogolea; na Hassiem Achmat, ambaye alinusurika kuuawa na papa aliyemshambulia akiwa baharini. Baadhi tu ya washiriki wakuu wa mashindano ya Paralympiki. Martine Wright, aliyenusurika mlipuko wa mabomu uliotokea London, Rim Ju Song, mshiriki wa kwanza kutokea Korea Kaskazini ambaye, miezi michache iliyipita, hakuweza kuogolea; na Hassiem Achmat, ambaye alinusurika kuuawa na papa aliyemshambulia akiwa baharini. Baadhi tu ya washiriki wakuu wa mashindano ya Paralympiki.

Ghana: Tangazo la Kibaguzi la Kombe la Dunia

Sokari anaandika kuhusu tangazo la biashara la Kombe la Dunia la kibaguzi lililotengenezwa na wakodishaji wa magari wa Kijerumani SIXT: “Tangazo hilo hapo juu lilitumwa kwangu na rafiki kutoka Ujerumani ambaye alifafanua hivi: Linacheza kauli mbiu kadhaa zenye mtazamo wa kiUlaya, mtazamo unaodharau Uafrika kuhusiana na mchezo wa mpira unaokuja...