Habari kuhusu Wakimbizi
Video Ioneshayo Mtoto Akiokolewa Kutoka Kwenye Kifusi cha Jengo Lililolipuliwa kwa Bomu Nchini Syria
Bomu lililaharibu makazi ya Ghina na kupelekea kifo cha mama yake. Aliweza kuokolewa akiwa hai pamoja na kufukiwa na kifusi akiwa peke yake.
Mitandao ya Kijamii Yasaidia Kuikoa Côte d'Ivoire Iliyokumbwa na Mafuriko
Abidjan na maeneo mengine ya Côte d'Ivoire yamekumbwa na mafuriko makubwa katika majuma kadhaa yaliyopita [fr]. Wakazi wa maeneo husika walijipanga kwenye mitandao ya kijamii ili kusaidia namna ya kuwaokoa wananchi waliokuwa wamekwama kwenye janga hilo. Kwenye mtandao wa twita na facebook, #CIVSOCIAL ilikuwa ni alama ishara iliyokuwa ikitumika kwa...
Simulizi la Kusikitisha la Ibrahim na Djouma wa Jamhuri ya Afrika ya Kati
Djouma na Amadou Moussa ni wazazi wa Ibrahim. Djouma na Ibahim ni wahanga wa shambulizi la kikatili lililofanywa na wanamgambo waaasi, tukio lililokatisha maisha ya ndugu watano wa damu katika Jamhuri ya Afrika ya Kati, karibu na mpaka wa Kameruni. Wanamgambo hao walikuja wakati Amadou Moussa akiwa mbali na nyumbani kwake....
Mapigano ya Wanakijiji Kugombea Ardhi Yasababisha Maafa Nchini Madagaska
Blogu ya L'Express Mada ilitoa taarifa kwamba kijiji kizima cha Andranondambo kilichoko Kusini mwa Madagascar kiliharibiwa [fr] kufuatia mapigano ya wanakijiji yaliyosababishwa na mzozo wa kumiliki ardhi. Vita vya wenyewe kwa wenyewe, ambayo ilidumu kwa siku tatu kati ya Mei 20-22, ilipoteza maisha ya wanakijiji wote. Akikumbuka tukio hilo, mmoja...
Baada ya Miezi Sita, Waathirika wa Kimbunga Haiyan Waendelea Kudai Msaada na Haki
Miezi sita baada ya kimbunga kikubwa kuharibu mamiliaoni ya makazi katika eneo la katikati ya Ufilipino, wahanga wanaendelea kuomba misaada na kutendelewa haki. Kuna madai ya kukosekana kwa mpango wa kurejesha hali kuwa ya kawaida.
Kwa nini Rwanda Inaituhumu Ufaransa Kusaidia Mauaji ya Kimbari ya 1994
Wakati Rwanda ikiwakumbuka waathirika wa mauaji ya kimbari yalitokea miaka 20 iliyopita, Rais Kagame anasema tena kuwa Ufaransa lazima “ikabiliane na ukweli mgumu” wa kukiri kushiriki kwenye mauaji hayo ya mwaka 1994 [fr]. Kama matokeo ya matamshi hayo, serikali ya Ufaransa imesusia matukio yote ya kukumbuka mauaji hayo na waziri...
Walebanoni Wazindua Kampeni ya Kuwatetea Wasyria Dhidi ya Ubaguzi wa Rangi
Watu wa Lebanon wameshikamana kutoa mwito wa kumaliza ubaguzi wa rangi dhidi ya wakimbizi wa Wasyria wanaoishi nchini humo, anaandika Joey Ayoub. "Nyumbani kwetu, ni kwenu," wanasema.
Ukuta Wetu wa Berlin Nchini Syria
"Wanafunzi wa Syria kwa mustakabali bora" ni blogu ya wnafunzi wa Syria wanaofadhiliwa, ambao wanaitumia kujadili matumaini yao, kukumbuka nyumbani, wasiwasi, mashaka, mitazamo chanya na matumaini kwa Syria iliyo bora.
Global Voices Yaanzisha Ushirikiano na Shirika la Kukutanisha Wakimbizi
We're proud to assist Refugees United with translation and local advice as they help families who have lost each other reconnect online.
Video: Usambazaji Vyakula katika Kambi ya Yarmouk-Syria
Shirika la habari la FAJER liliweka mtandaoni video ya kambi ya wakimbizi ya Yarmouk mjini Damascus wakati wa kupokea mgawo wa chakula cha kuwalisha wakazi 18,000 wa kambi waliobaki, ambao wamelazimishwa kula wanyama waliopotea ili kuokoa maisha yao wakati huu ambapo kuna uhaba mkubwa wa chakula. Video ni ya tarehe...