Habari kuhusu Siasa kutoka Aprili, 2014
Rais Mugabe Anadhani Naijeria Inanuka Ufisadi Kuliko Zimbabwe
"#Mugabe ana ujasiri wa kuiita serikali ya Naijeria kuwa imekithiri ufisadi. Serikali ya Naijeria ina haki ya kijisikia kutukanwa."
Asilimia 20-40% ya Fedha Katika Sekta ya Maji Barani Afrika Hupotelea kwa Utoaji Rushwa
Mustapha Sesay, Balozi wa Uadilifu wa Afrika Magharibi aliandika kuhusu ufisadi katika sekta ya maji kwenye mtandao wa Waandishi wa Habari wa WASH wa Afrika Magharibi : Suala la upatikanaji wa maji safi na kwa bei nafuu ni haki ya kibinadamu lakini hii haijapewa kipaumbele inavyohitajika sana. Utoaji rushwa katika...
Mgogoro Usiopewa Uzito Stahiki Nchini Burundi
Wakati nchi jirani ya Rwanda inagonga vichwa vya habari na maadhimisho ya mauaji ya kimbari ya mwaka wa 1994 na kuongezeka kwa mvutano na Ufaransa, Burundi imeharibiwa katika kupuuzwa kwa mgogoro wa kisiasa na dalili za vurugu zinazoweza kusababisha mapigano mapya ya Wahutu na Watutsi. Tshitenge Lubabu nchini Burundi anatoa...
Wa-Macedonia Wamcheka Rais wao ‘Kuchemka’ Kwenye Mahojiano
Wakati uchaguzi wa Rais Macedonia unakaribia, makosa aliyoyafanya Rais wa Macedonia Gjorge Ivanov kwenye mahojiano ya televisheni yasababisha majadala mkali miongoni mwa watumiaji wa mitandao ya kijamii
Kwa Nini Rais wa Madagaska Hajatangaza Uteuzi wa Waziri Mkuu
Rais mpya wa Madagaska Hery Rajaonarimampianina alichaguliwa kuwa raia mnamo Desemba 20, 2013. Miezi michache baadae, bado hajatangaza uteuzi wa waziri mkuu wa serikali yake mpya. Wachunguzi wengi wanashangaa kwa nini imechukua muda mrefu. Mwanablogu wa Kimalagasi Michael Rakotoarison ana maoni tofauti kuhusiana na hali hiyo; hoja yake ni kuwa huenda...
Kwa nini Rwanda Inaituhumu Ufaransa Kusaidia Mauaji ya Kimbari ya 1994
Wakati Rwanda ikiwakumbuka waathirika wa mauaji ya kimbari yalitokea miaka 20 iliyopita, Rais Kagame anasema tena kuwa Ufaransa lazima “ikabiliane na ukweli mgumu” wa kukiri kushiriki kwenye mauaji hayo ya mwaka 1994 [fr]. Kama matokeo ya matamshi hayo, serikali ya Ufaransa imesusia matukio yote ya kukumbuka mauaji hayo na waziri...
Uchaguzi Mkuu wa India 2014: Kampeni Kwenye Mitandao ya Kijamii
Mitandao ya kijamii imekuwa ni sehemu ya ugunduzi na ubunifu. Milind Deora [Waziri wa Muungano na Mbunge wa Mumbai Kusini] anatamba kuwa mgombea wa kwanza kupatikana kwa wapiga kura wake kwenye mtandao wa WhatsApp na BBM, na huko anajadili mpango kazi wake ikiwa ni pamoja na shughuli zake na mipango...
Waethiopia Waadhimisha Siku ya Wajinga kwa Kuikejeli Televisheni ya Taifa
"Katika kujibu shutuma za wanaharakati hao siku hiyo, #ETv walitangaza kuwa hii [siku ya wajinga] ndio siku pekee ambayo hawaimiliki"
Jiunge na IGF Japan Kujadili Utawala wa Mtandao
IGF Japan, hatua ya maendeleo nchini Japani ya Jukwaa la Utawala Mtandao, ambapo watu wanaojihusisha mtandaoni huja pamoja kujadili changamoto za utawala wa mtandao, ulifanyika Machi 14, 2014
Utafiti wa Wenyeji katika Chuo cha Bahamas
Akifuatilia posti yake kuhusu “ujinga wa kupunguza bajeti kwa Chuo cha Bahamas”, Blogworld anasema: Si tu kwamba chuo hicho ni taasisi ya taifa ya elimu ya juu, lakini ndio taasisi pekee ya umma kwa wenyeji ambayo inahusiana na aina yoyote ya utafiti unaoendelea katika nchi ya Bahama.