· Februari, 2014

Habari kuhusu Siasa kutoka Februari, 2014

Pongezi kwa Waziri Mkuu Mpya wa Nepal

  23 Februari 2014

Bunge la Nepal limemchagua Bw. Sushil Koirala (75), rais wa chama cha Nepali Congress, kuwa Waziri Mkuu wa Nepal. Mwanablogu wa NNepali aishiye ughaibuni Indra anampongeza Waziri Mkuu mpya na anafikiri kwamba “zawadi aliyonayo Bw. Koirala kwa kuwawezesha wengine kwa unyenyekevu na ukweli haitaondoka wa haraka”.

Kiongozi wa Upinzani Nchini Venezuela Leopoldo López Ajisalimisha Serikalini

  20 Februari 2014

Kiongozi wa Upinzani nchini Venezuela Leopoldo López amejisalimisha mwenyewe kwa Vikosi vya Polisi, kama alivyokuwa ametangaza angefanya kwenye video [es] hiyo hapo juu. López, kiongozi wa chama cha Voluntad Popular, alitakiwa  kujisalimisha kwa agizo la mahakama jijini Caracas kwa kutuhumiwa kuhusika na makosa ya jinai yanayohusiana na maandamano  yanayoendelea nchini...