Habari kuhusu Siasa kutoka Juni, 2015
Abel Wabela: “Kupambana na Hali ya Kutokuchukua Hatua na Kutojali…Hii Ndio Nia Yangu Kama Mwanadamu”
"Maangalizo, vitisho, kukamatwa na mateso hakujanifanya kuacha kutumia haki zangu za msingi za kujieleza," anasema Abel Wabela, mmoja wa wanablogu wa Zone9 wa nchini Ethiopia ambao walifungwa gerezani tangu Aprili 2014.
Alama ya #AchaHofu Yatumika Kufuatilia Uchaguzi wa Mexico
Wakati wa uchaguzi wa Jumapili iliyopita nchini Mexico, taasisi ya kulinda uhuru wa kujieleza, ARTICLE 19 iliendesha kampeni ya #RompeElMiedo (#AchaHofu) kwa lengo la kufuatilia usalama wa waandishi wa habari
Raia wa Uganda Wanataniana kwa Mgogoro ‘wa Kawaida’ wa Awamu ya Tatu Burundi
Maandamano makubwa na mapinduzi yaliyoshindwa vyote vlitokea kwa sababu ya Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza kutaka kugombea kwa awamu ya tatu. Rais wa Uganda anaangalia uwezekano wa kugombea muhula wa tano.
Muda Gani Umebaki kwa ‘Marais wa Maisha’ Barani Afrika?
Matukio nchini Burundi na nchi nyinine kama Kongo (DRC), Burkina Faso na Rwanda yameendeleza mjadala wa muda mrefu barani Afrika kuhusu ukomo wa madaraka
Kampeni ya Kujipiga Picha Yaongeza Uvumilivu wa Kidini na Kupunguza Ukabila Nchini Myanmar
"Yeye ni Msikh na mie Mwislamu. Lakini tu marafiki. Ingawa tuna tofauti zetu, bado tunaweza kuzungumzia mitazamo na imani zetu, na kuzikubali na kuziheshimu tofauti zetu."
Ramani Hizi Zaonesha Mahali Walipotesewa na Kuuawa Wanahabari wa Kambodia
Kituo cha Haki za Binadamu cha kambodia kimezindua jarida linaloelezea ukiukwaji wa haki za binadamu unaofanywa kwa waandishi wa habari nchini Kambodia. Katiba ya nchini Kambodia inatoa uhuru wa kupashana habari lakini wanahabari wanazidi kunyanyaswa na kuuawa, hususani kwa waandishi wanaopasha habari kuhusiana na ukiukwaji wa maadili unaofanywa na maafisa...