Habari kuhusu Siasa kutoka Julai, 2014
Hotuba ya Ushindi ya Rais Mteule wa Indonesia
Rais mteule wa Indonesia Joko Widodo or Jokowi alitoa hotuba ya ushindi akitambua moyo wa kujitolea ulioonyeshwa na wananchi: Uchaguzi huu wa rais umechochea mtazamo mpya chanya kwetu, na kwa taifa letu kwa ujumla. Uhuru wa watu na uwajibikaji wa kisiasa vinashamiri katika nyoyo za kizazi kipya. Moyo wa kujitolea...
Trinidad & Tobago: Je, Kuishi kwenye Enzi za Kidijitali Kunahatarisha Haki yako ya Faragha??
Blogu ya ICT Pulse inapitia taarifa iliyochapishwa hivi karibuni iliyoandaliwa na Tume ya Umoja wa Mataifa ya Haki za Binadamu juu ya haki ya faragha katika enzi hizi za dijitali.
Miezi Michache Baada ya Kupotea kwa MH370, Kuanguka kwa Ndege Nchini Ukraine Kwawashitua Raia wa Malasia
Mhudumu wa ndege wa Malaysia aelezea katika Instagram na Twita kuhusiana na watu wengi kupoteza maisha katika matukio ya ajali za ndege za Malaysia: "Katika kipindi cha miezi minne niliwapoteza marafiki zangu takribani 30."
Matamshi Matano ya Kushangaza Kufuatia Kuanguka kwa Ndege MH17 Nchini Ukraine
Wakati kukiwa na hisia zinazozidi kuongezeka kufuatia kuanguka kwa ndege nchi Ukraine, matamshi kadhaa yaliyotolewa na watu maarufu Moscow na Donetsk yamevuta hisia za watu
Rais wa Zambia Ajaribu Kuthibitisha Kuwa Yuko ‘Fiti’ kwa Picha Hizi za Facebook. Baadhi Hawajashawishika
Raia wa Zambia wanaendelea kuwa na wasiwasi wa safari za kimya kimya anazofanya Rais Sata nje ya nje, ambazo zimekuwa zikiitwa na serikali kuwa likizo za kikazi
Wa-Indonesia Wawasha Mishumaa Elfu Moja Ishara ya Amani kwa Palestina
Raia wa Indonesia walikusanyika katikati ya Jakarta, mji mkuu wa nchi hiyo, kuwasha mishumaa 1,000 kupinga mashambulio ya Israel katika ukanda wa Gaza. Indonesia ni moja ya nchi maarufu zaidi kwa wingi wa waumini wa dini ya Kiislam.
Waandishi wa kimataifa Wakashifu Israeli kwa Kuendelea kwa Ujenzi wa Makazi
Waandishi kumi na sita wa kimataifa ambao walishiriki katika Tamasha la Wapalestina la Fasihi, lililofanyika katika miji kadhaa Palestina kuanzia Mei 31 hadi Juni 5, walitoa taarifa kukashifu Israeli kwa kuendelea kwa ujenzi wa makazi na kupongeza juhudi za kususia kampeni ya Boycott Divest and Sanction (BDS). Taarifa, kupitia mtandao...
Baada ya Kuchoshwa na Kudorora kwa Uchumi, Wa-Ghana Waanzisha Harakati
Hali ya ghadhabu dhidi ya serikali ilitokana na ongezeko la haraka la kushuka kwa thamani ya fedha ya Ghana pamoja na kukosekana kwa mafuta vituoni hali iliyopelekea kuwa na misururu mikubwa ya watu katika vituo vya mafuta ya petroli
Mfungo wa Ramadhani Wawaingiza Watu Matatani kwa Kula Daku Usiku Nchini Misri
Vijana kumi na moja walikamatwa nchini Misri wakiwa wanapata daku usiku, kitendo kinachochukuliwa kuwa kosa la kukutana usiku kinyume na sheria. Noor Mattar ana taarifa zaidi kuhusu mahabusu hao wa 'kosa la kula daku' kinyume cha sheria.
Mjadala Kuhusu Upatikanaji wa Mtandao wa Intaneti Wazidi Kushika Kasi Nchini Cuba
Raia wa nchini Cuba waendelea kudai kupunguzwa kwa gharama za mtandao wa intaneti pamoja na urahisi wa upatikanaji wake.