Habari kuhusu Siasa kutoka Agosti, 2013
Mapigano Yalipuka Msikitini Baada ya Mhubiri Kumlaani el-Sisi
Mapigano, yaliyowekwa kwenye mtandao wa YouTube, yamesambazwa sana na kuzua gumzo kubwa mtandaoni.
Iran: Mwanablogu Aliyefungwa Jela Afanya Mgomo wa Kutokula
Hossein Ronaghi Malki mwanablogu anayetumikia kifungo cha miaka 15 jela alianza mgomo wake wa kutokula kuanzia wiki iliyopita. Kwenye mtandao wa Facebook kampeni imeanzishwa yenye lengo la kummwuunga mkono.
Makanisa Yashambuliwa Nchini Misri
David Degner aweka picha kutoka makanisa yaliyoshambuliwa na kuchomwa katika sehemu iitwayo Mallawi, Minya, Misri ya Juu hapa. Anaandika: Siku ya Ijumaa makanisa mawili katika kijiji cha Mallawi, jimbo la Minya, yalishambuliwa na kuchomwa moto. Baada ya mashambulizi dhidi ya wafuasi wa Morsy ambapo zaidi ya watu 600 walifariki, wafuasi wa Morsy walikusanyika baada...
Serikali ya Uzbeki Yatafuta Namna ya Kudhibiti Wanablogu
Serikali nchini Uzbekistan inatafuta namna ya kutumia hatua kali za kudhibiti wanablogu wa nchi hiyo. Alisher Abdugofurov kwenye Registan.net anajadili sababu ya kutokea hali hii katika jamii ambayo haina wanablogu wengi wa kuanzia zoezi hilo.
Iran: Waziri Mpya wa Kigeni Yupo Kwenye Mtandao wa Facebook
Waziri mpya wa Uhusiano wa Kimataifa wa Iran Mohammad Javad Zarif ana ukurasa wa Facebook ambapo huutumia kujibu maswali. Anasema “Mimi na watoto wangu huuhuisha (kuweka habari mpya) ukurasa huu.” Ukurasa huo una zaidi ya wafuatialiaji 79,854 walioupenda (wakati wa kutafsiriwa kwa posti hii). Mtandao wa Facebook hudhibitiwa nchini Iran lakini ndio...
Zimbabwe: Robert Mugabe Ashinda Uchaguzi, Atuhumiwa Kuiba Kura
Daftari la wapiga kura la Zimbabwe lilisemekana kuwa na watu milioni mbili waliokufa. Botswana imetoa wito wa kukaguliwa kwa matokeo ya uchaguzi.