· Julai, 2013

Habari kuhusu Siasa kutoka Julai, 2013

Hali ya Uislamu Katika Asia ya Kusini

  27 Julai 2013

Murray Hunter wa Chuo Kikuu cha Malaysia Perlis anajadili hali ya jamii ya Kiislamu katika Asia ya Kusini pamoja na masuala yanayohusiana na kukua kwa Uislamu katika eneo hilo. Umaskini, kujua kusoma na kuandika, elimu, kuhamishwa, ukabaila, ukosefu wa ajira, ukandamizaji, na udhibiti ni mambo yanayowaonea Waislamu ndani ya ASEAN. Serikali pamoja na...

Maandamano ya Kudai Uchaguzi nchini Madagaska Yasababisha Vurugu

Blogu ya Vola R ya Ma-Laza inaandika kwamba watu 7 walijeruhiwa [fr] kufuatia matumizi ya nguvu yaliyofanywa na polisi dhidi ya waandamanaji waliokuwa wanadai kufanyika kwa uchaguzi mjini Antananarivo, Madagaska. Chama kinachoongoza maandamano kinasema kwamba utawala uliopo hauna dhamira ya kuitisha uchaguzi mwaka huu na kwamba serikali imeng'ang'ania madarakani. Kiongozi wa...

Mwana-Habari Menna Alaa Ashambuliwa na Wafuasi wa Morsi

Mwanablogu na mwanahabari wa video Menna Alaa leo hii ameshambuliwa na waandamanaji wenye hasira wanaomwunga mkono Morsi. Mwanablogu huyo ameweka ushuhuda wake kwa lugha ya kiingereza kwenye makala hii iliyo katika blogu inayokusanya matukio nchini Misri iitwayo Egyptian Chronicles. Anaandika: Kofi nililopigwa usoni, alama iliyobaki usoni mwangu pamoja na kuibwa...

Al Jazeera Yatuhumiwa Kutangaza “Habari za Upendeleo”

Al Jazeera iko kwenye wakati mgumu nchini Misri kwa kile kinachoelezwa na wengi kuwa ni "upendeleo" wake katika kutangaza habari zake wakati na baada ya kuondolewa madarakani kwa rais wa zamani wa Misri Mohamed Morsi mnamo Julai 4. Kituo hicho cha televisheni kilichopo nchini Qatar kinatuhumiwa kuegemea upande wa wafuasi wa Muslim Brotherhood na kimegeuka kuwa mdomo wa kikundi hicho.