Habari kuhusu Siasa kutoka Juni, 2012
Misri: Yatambulisha Kipimio cha Morsi
Baada ya miaka 32 ya Hosni Mubarak, Misri imepata rais mpya Mohamed Morsi, na pia kitumizi cha kufuatilia utendaji pamoja na maendeleo ya kutimiza ahadi kuu 64 alizozitoa rais huyo mteule wakati wa kampeni za uchaguzi nchini humo.
Sudani: Kuondoa kizuizi cha Mapinduzi ya Sudani
Tofauti na nchi nyingine katika eneo lake, Sudani mara nyingi huwa haipati nafasi katika vyombo vikuu vya habari, na hili lilikuwa wazi zaidi wakati wa maandamano yalifanyika Ijumaa na Jumamosi. Sababu ni kwamba serikali ya Sudani imevibana mno vyombo vya ndani vya habari na kuwazuia waandishi kuripoti habari zinazohusu masuala ya haki za binadamu na ufisadi.
Sudani: “Polisi Yakanusha Kutumia Risasi; Majeruhi wote ni Wakufikirika
Maafisa wa serikali ya sudani wanarudia ‘uongo’ uliozoeleka ambao watawala wa ki-Arabu wamekuwa wakitumia tangu kuanza kwa yale yanayoitwa Mapinduzi ya Uarabuni yaliyoanza mwezi Desemba 2010. Imekuwa kawaida kusikia kauli kama, ‘waandamanaji wamedhibitiwa wakati wakiwashambulia polisi, ambao nao walijihami kwa kushambulia' Watumiaji wa mtandao wanaonyesha picha tofauti wakati tetesi zinadai mtandao wa intaneti utakatwa kufuatia kuongezeka kwa maandamano.
Sudani: Watumia Mtandao Wathibitisha Tetesi za Kukatwa kwa Intaneti
Raia wa kwenye mtandao wanaifuatilia kwa karibu Sudani, kufuatia tetesi kuwa serikali ya Sudani inadhamiria kuukata mtandao wa intaneti - hatua inayokumbushia jaribio la Misri kuwanyamazisha wanaharakati na kuthibiti mapinduzi ya Januari 25 pale ilipoondoa uwezekano wa watu kuwasiliana kwa mtandao wa intanenti mnamo Januari 27.
India: Kipindi cha Runinga cha Aamir Khan Chaweka Wazi Masuala ya Kijamii
Kipindi kipya cha maongezi kwenye televisheni nchi India kinachoitwa Satyamev Jayate (Ni Ukweli tu Utakaoshinda) kinachoendeshwa na muigizaji na mtengeneza filamu wa Bollywood, Aamir Khan kinaleta na kujadili miiko na masuala moto moto ya kijamii ambayo yanawanasa na kuwavutia WaHaindi wengi zaidi na zaidi. Wananchi wa kwenye mtandao wanatoa maoni yao.
Ethiopia: Ardhi, Historia na Haki katika Eneo la Gambella
Wanaharakati wa masuala ya ardhi wanatumia hati ya malalamiko ya mtandao, mtandao wa facebook na twita kufanya kampeni dhidi ya unyang’anyi wa ardhi nchini Ethiopia. Inaarifiwa kwamba wanakijiji kwenye jimbo msikini zaidi nchini humo, Gambella, wanalazimishwa kuhamia kwenye vijiji vilivyobuniwa na serikali ili kuwapisha wanaoitwa 'wawekezaji' wakubwa.
Kenya: Wanaharakati wapigana vita dhidi ya ufisadi kwa intaneti
I Paid a Bribe ni njia mojawapo inayotumiwa na wanaharakati dhidi ya ufisadi nchini, kwa kutumia teknolojia mpya ili kuwawezesha kupata ripoti za utoaji wa hongo.' I paid a Bribe' imefuatia muundo wa ‘India Anti-Corruption Portal (IPAB)' na ni ushirkiano kati ya IPAB na Wamani Trust ya Kenya ili kuleta IPAB katika Afrika Mashariki na Kati.
Uganda: Je, Uganda inageuka kuwa dola ya kifalme?
Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni amekuwa madarakani tangu mwaka 1986. Majuma machache yaliyopita, wananchi walianza kudodosa habari za nani hasa atamrithi kama ataamua kutokugombea kwa awamu ya nne mwaka 2016. Tetesi zinadai kwamba rais anamwunga mkono mkewe, Waziri wa mambo ya Karamoja kurithi kiti cha rais.
Lesotho: Uchaguzi wa amani ambao hukuusikia
Lesotho, nchi ndogo inayozungukwa na Afrika Kusini pande zote, ilifanya uchaguzi wa wabunge Jumapili, uchaguzi ulioendeshwa kwa utulivu, lakini uchaguzi huo haukupewa uzito na vyombo vikuu vya habari.