· Januari, 2011

Habari kuhusu Siasa kutoka Januari, 2011

Dunia ya Uarabu: “Acheni Kulia Juu Sudani”

  31 Januari 2011

Kura ya maoni kwa ajili ya uhuru wa Sudani ya Kusini leo imeiweka nchi hiyo kwenye uangalizi wa karibu miongoni mwa watumiaji wa twita wa Kiarabu. Kuanzia Saudi Arabia mpaka Palestina, watumiaji Twita wa Kiarabu wanajadiliana kuhusu mshikamano, kugawanyika na rasili mali za Sudani.

Syria: Propaganda ya Vyombo vya Habari vya Serikali Kuhusu Maandamano ya Tunisia na Misri

Mwanablogu wa ki-Syria Maurice Aaek amegundua[ar] kwamba vyombo vya habari vinavyoendeshwa na serikali nchini Syria vinachapisha habari za uongo na nusu-kweli kuhusu maandamano ya upinzani nchini Tunisia na Misri. Amegundua kwamba gazeti la Tishreen daily halikuweka sababu ambazo zilimfanya Ben Ali aondoke na kuwaachia watu wajitafsirie wenyewe, na kuwa gazeti...

Sudan: Muda mfupi Kuelekea Kwenye Kura ya Maamuzi ya Sudani ya Kusini

Sudani ya Kusini itaendesha kura ya maoni ili kuamua ikiwa iendelee kubaki kuwa sehemu ya Sudani ama la ifikapo tarehe 9 Januari 2011. Kuna uwezekano ni mkubwa kuwa nchi hiyo kubwa zaidi katika bara la Afrika itagawanyika kuwa nchi mbili zinazojitegemea. Hapa ni maoni ya hivi karibuni zaidi kwenye makala za blogu kuhusu kura hiyo ya maoni. Southern Sudan will hold a referendum on whether or not it should remain as a part of Sudan on 9 January 2011. It is most likely that Africa's largest country will split into two. Here's our latest roundup of blog posts about the referendum. Southern Sudan will hold a referendum on whether or not it should remain as a part of Sudan on 9 January 2011. It is most likely that Africa's largest country will split into two. Here's our latest roundup of blog posts about the referendum.

Tunisia: Anonymous Dhidi ya Ammar – Nani Atashinda Vita ya Kuchuja Habari?

Kichuja habari cha Tunisia, kinachojulikana kama Ammar, kinaeendelea kutishia kuziharibu na kuzifunga anuani za wanaharakati wa mtandaoni, katika nchi hiyo ambayo imekuwa ikishuhudia wimbi la maandamano tangu katikati ya mwezi Desemba. Ni leo tu, wanaharakati wamedai kwamba serikali imeingilia anuani zao za barua pepe,na kuziingilia blogu na mitandao yao ya kijamii, na kuzizuia zisifanye kazi. Hatua hii inaonekana kuja kama kulipiza kisasi kwa shambulio lililofanywa na kikundi cha wanaharakati wa mtanda0ni wanaojulikana kama Anonymous, ambalo lililenga njia na mitandao ya muhimu ya Serikali ya Tunisia.