Habari kuhusu Siasa kutoka Septemba, 2010
Colombia: maoni ya Awali Kuhusu Kifo cha Kiongozi wa FARC ‘Mono Jojoy’
Víctor Julio Suárez, ambaye anajulikana zaidi kama Jorge Briceño or Mono Jojoy, mmoja wa viongozi wa juu wa Majeshi ya Ukombozi wa Colombia (FARC), aliuwawa katika kile kilichoitwa "Operesheni Sodoma." Watumiaji wa Twita wa Colombia walianza mara moja kuandika maoni yao kuhusu habari hiyo.
Irani: Huenda Mwanablogu Aliyefungwa, Hossein Derakhshan (”Hoder”), Akakabiliwa na Hukumu ya Kifo
Mwendesha mashtaka huko Tehrani anataka mwanablogu wa Irani aliye gerezani Hossein Derakhshan ("Hoder") apewe adhabu ya kifo. Hakimu bado hajatoa uamuzi. Derakhshan anashtakiwa kwa kosa la “kushirikiana na dola adui, kutangeneza propaganda dhidi ya utawala wa Kiislamu, kutusi utukufu wa dini, na kutengeneza propaganda kwa ajili ya matumizi ya vikundi vinavyopinga mapinduzi." Alitiwa nguvuni miezi 22 iliyopita.
Brazil: Uchaguzi Safi kwa Mtindo wa “Jifanyie Mwenyewe”
Chini ya mwezi mmoja ujao kutakuwa na uchaguzi nchini Brazil na mradi wa Eleitor 2010 tayari umekwisha kuwa na nguvu za kubadili mchakato huo: ni mradi wa “vyanzo vya habari vya kiraia” ambao una lengo la kuratibu taarifa za raia zinazoripoti ukiukwaji wa mchakato wa uchaguzi nchini Brazil. Kwa kupitia jukwaa hilo, kuna simulisi kadhaa za kuburudisha ambazo zimeshaanza kujitokeza.
Msumbiji: Maputo katika Hali ya Tahadhari Kutokana na Machafuko
Jiji la Maputo lipo kwenye hali ya tahadhari wakati machafuko yakisambaa kutokana na kupanda kwa bei ya mkate, maji na umeme. Wakazi wanataarifu kuwepo kwa vurugu mitaani huku hali ikizidi kuwa mbaya.