· Novemba, 2009

Habari kuhusu Siasa kutoka Novemba, 2009

Ufaransa: Tuzo ya Fasihi Yaja na Masharti

  19 Novemba 2009

Mwanzo wa msimu wa Fasihi ya Kifaransa mwaka huu ulishuhudia mwandishi wa riwaya na michezo ya kuigiza mwenye asili ya Kisenegali na Kifaransa Marie N’Diaye akipewa tuzo iliyosuburiwa sana ya Prix Goncourt. Lakini, N’Diaye na familia yake walikwishahamia mjini Berlin miaka miwili iliyopita, hasa kutokana na siasa za rais wa Ufaransa Nicolas Sarkozy. Mwaka jana, jopo la tuzo hii yenye hadhi walizusha hisia kali pale walipomchagua mwandishi wa Kiafghani Atim Rahimi, kwa kitabu chake cha Kifaransa, Syngué Sabour. Je hii itakuwa ni fursa nyingine ya kusherehekea mchanganyiko wa aina mbalimbali katika jamii inayobadilika ya Kifaransa? Au itakuwa ni wasaa utakaoharibiwa na utete wa tukio?

Misri: Haki ya Kijerumani kwa Marwa El Sherbini

Muuaji wa Marwa El-Sherbini, mwanamke wa Kimisri ambaye alichomwa visu mpaka kufa na muhamiaji mwenye asili ya Urusi na Ujerumani, Alex Wiens, ndani ya mahakama huko Ujerumani, amehukumiwa kifungo cha maisha, bila uwezekano wa kuachiwa mapema. Haki hatimaye imetolewa na muuaji anaadhibiwa, wanasema wanablogu wa Misri.

Video: Dunia Yaadhimisha Kuanguka kwa Ukuta wa Berlini

  11 Novemba 2009

Leo ni Kumbukumbu ya 20 ya kuanguka kwa Ukuta wa Berlini, kizingiti madhubuti cha kiusalama ambacho kiliwahi kuligawa jiji la Berlini katika pande mbili za Mashariki na Magharibi huko Ujerumani. Leo tunaonyesha baadhi ya picha za video zinazotoka pande mbalimbali za dunia zinazopandishwa ili kusherehekea siku hii na nini ukuta huo ulimaanisha siyo Ujerumani tu bali duniani kote.

Irani: Vuguvugu la Kijani Laupinga Utawala Tena

Upande wa upinzani wa Vuguvugu la Kijani nchini Irani mnamo tarehe 4 Novemba uliendesha maandamano makubwa ambapo maandamano hayo yalikabiliwa na matumizi makubwa ya nguvu ya kuyazuia yaliyofanywa na vikosi vya usalma. Kama ambavyo sasa inatarajiwa, uandishi wa habari wa kiraia nchini Irani haukukosa kitu kwani ulirekodi 'historia' hiyo kupitia simu zao za mikononi.