Habari kuhusu Uhamiaji na Uhamaji kutoka Agosti, 2012
Kocha wa Timu ya Taifa ya Zambia Atunukiwa Ukaazi wa Kudumu
Zambia imewahi kuwa na makocha wengi wa kigeni wa timu ya Taifa ya soka, lakini ni Mfaransa Herve Renard, aliyeongoza timu hiyo hadi kushina Kombe la Washindi Barani Afrika mwaka 2012, aliyepata upendeleo wa pekee. Ili kutambua mafanikio yake haya, serikali imemtunuku ukaazi wa kudumu lakini uamuzi huo unaonekana kuwekewa chumvi ya kisiasa.