Habari kuhusu Fasihi
Trinidad na Tobago: Washindi wa Tuzo za Hollick Arvon
Blogu ya Bocas Lit Fest imewatangaza waandishi chipukizi kutoka Jamaica, Grenada, St. Vincent na Trinidad na Tobago kuwa washindi wa Tuzo zinazovuta watu wengi za Waandishi wa nchi za Karibiani za Hollick Arvon kwa mwaka 2014, ambazo kwa mwaka huu zilifanyika kwa mara ya pili.
Fasiri ya Lugha ya Kikannada ya Karne ya 11 Yapatikana kwenye Mfumo wa Wikisource
Vachana Sahitya ni aina ya uandishi kwa mtindo wa sauti katika lugha ya ki-Kannada ambao ulianzia karne ya 11 na kukua sana kwenye karne ya 12. Makala ya Subhashish Panigrahi inaripoti (ikiwa imeandikwa kwa ushirikiano wa Pavithra Hanchagaiah na Omshivaprakash) kwenye blogu ya Wikimedia kwamba waandishi wawili wa Wikimedia wakishirikiana...
Uajemi: Washairi Wawili Watiwa Nguvuni
Washairi Mehdi Mousavi na Fatemeh Ekhtesari wametokomea nchini Uajemi. Kwa mujibu wa taarifa za habari, washairi hao wamewekwa kizuizini tangu mwanzoni wa mwezi Desemba. Zaidi ya watu mia mbili wametia saini hati ya malalamiko mtandaoni na kutoa wito kwa Umoja wa Mataifa kuchukua hatua kuhusiana na hali za wanaharakati wa...
Vijiwe Vya Usomaji Gazeti Mjini Mumbai Vyazorota
Vachanalays (vituo vya kusoma magazeti) ni jambo la kawaida katika vitongoji vingi mjini Bombay ambapo wenyeji husoma magazeti na kujadili habari zilizotokea siku husika. Sans Serif anaripoti jinsi vituo hivyo vinavyozidi kupitwa na wakati pole pole. Blogu hiyo pia inaonyesha picha nzuri inayojieleza ya mwanablogu wa picha M.S. Gopal juu ya maudhui hayo...
Kitabu-pepe Kipya cha GV: Sauti ya Kiafrika ya Matumaini na Mabadiliko
"Sauti ya Kiafrika ya Matumaini na Mabadiliko", kinakupa mtazamano wa kipekee kuhusu watu na habari za eneo la Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara kupitia posti zetu zilizo bora zilizoandikwa kwa lugha ya Kiingereza kwa mwaka 2012. Hii ni zawadi sahihi kabisa ya kuukaribisha mwaka mpya.
Mexico: Uandishi Kutoka Gerezani
Enrique Aranda Ochoa writes literature from jail. Convicted of kidnapping in 1997 with a sentence of 50 years in prison, Enrique has used his time in jail to write six novels and earn various literature awards. His latest book, available for purchase in an electronic format, focuses on the mysteries of the Mayans.
Afrika: Tuzo la Mbuyu wa Dhahabu
Wasilisha kisa chako upate fursa kushinda Tuzo ya Mbuyu wa Dhahabu: “Tuzo ya Mbuyu wa Dhahabu ilianzishwa mwaka 2008 kuwahamasisha waandishi wa ki-Afarika waliojikita katika vitabu vya watoto na vijana.”
Mgogoro wa Umoja wa Ulaya: Kitabu cha Kwanza cha Global Voices cha Kieletroni
"Umoja wa Ulaya katika Mgogoro" (EU in Crisis) ni chapisho letu la kwanza katika Mradi wa Vitabu wa Global Voices na ambao unahusisha makala bora zaidi kuhusu mazungumzo ya kijamii, ushiriki na uhamasishaji unaopewa nguvu na raia wanaopitia nyakati ngumu za kubana matumizi katika bara la kale zaidi na kwingineko.
Peru: Kampeni ya Kuzuia Kufungwa kwa Maktaba ya Amazon
Juan Arellano wa Globalizado [es] anaripoti juu ya kampeni ya kuzuia kufungwa kwa maktaba huko Iquitos, Peru , maktaba ambayo inatilia mkazo vitabu na masuala yanayohusu Amazon. Maktaba hiyo ni ya pili kwa umuhimu katika masuala ya Amazon huko Marekani ya Latini.
Wapiga picha wa Kiafrika, waandishi na wasanii wapata sauti zao kwenye blogu
Kadri Waafrika wengi wanavyozidi kugundua nguvu ya kublogu kama zana ya kutoa maoni kwa kiwango cha dunia nzima, tarakimu ya wanablogu imeongezeka na pia maudhui yanayopewa kipaumbele. Kwa tarakimu hiyo ya kukua kwa blogu, wasanii wengi wa Kiafrika wamejiunga, na ongezeko kubwa likionekana kwenye blogu za mashairi kama ilivyo kwa upigaji picha unaochipukia na blogu za sanaa za maonyesho. Tunazipitia baadhi.