Habari kuhusu Sheria kutoka Februari, 2016
Mtumiaji wa Twita Nchini Saudi Arabia Ahukumiwa Kifungo cha Miaka 10 na Viboko 2,000 kwa Kosa la “Kukufuru Dini”

Saudi Arabia imemhukumu mtumiaji wa mtandao wa Twita kifungo cha miaka 10 jela pamoja na viboko 2,000 kwa kosa la kuandika twi 600 "zinazoeneza imani ya ukana-Mungu" mtandaoni.
Polisi wa Kidini Thelathini Nchini Saudi Arabia Wahitimu Mafunzo ya Kukabiliana na Uchawi
Wajumbe thelathini wa Tume ya Kusimamia Maadili na Kukabiliana na Maovu wamemaliza mafunzo ya siku tano ya namna ya kukabiliana na uchawi, kuwatambua walozi na hata kuvunja laana zao.