Habari kuhusu Sheria kutoka Septemba, 2012
Mbinu za Kugundua Dawa Bandia katika Nchi Zinazoendelea
Watu 700,000 hufa kila mwaka kwa kutumia dawa bandia za malaria na saratani pekee. Shirika la Afya Duniani, WHO linasema katika ripoti yake kuwa, mapato kutoka kwa dawa hizi kila mwaka hukaribia dola bilioni 200.
Pakistani: Msichana wa Kikristo wa Miaka 11 Awekwa Kizuizini kwa Kukashifu Dini.
Rimsha Masih msichana Mkristo mwenye umri wa miaka 11 ametuhumiwa kwa makosa ya kukashifu na ameshikiliwa kwa siku kumi na nne katika gereza za watoto huko Rawalpindi, nchini Pakistani. Anashitakiwa kwa kuchoma kurasa za kitabu cha Noorani Qaida, kinachotumika kwa wanafunzi wa lugha ya kiarabu, na kuziweka katika mfuko wa 'rambo'.