Habari kuhusu Sheria kutoka Julai, 2012
Tanzania: Mgomo wa Walimu Watikisa Nchi
Zikiwa zimebaki siku chache kabla ya kufanyika zoezi la sensa, walimu nchini Tanzania wako katika mgomo kuishinikiza serikali kuwalipa madai yao pamoja na kuboresha mishahara yao. Hatua hiyo imevuta hisia za watumiaji wengi wa mitandao ya kijamii wanaojadili madhara ya mgomo huo.
Togo: Muhubiri Asafirisha Kilo 4.2 za Madawa ya Kulevya Yaliyofichwa kwenye Pipi ‘k Build Church
Muhubiri wa Injili raia wa Togo, Woegna Yao Koufoualesse alikamatwa katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Accra akiwa na kiasi cha kilo 4.2 za madawa ya kulevya aina ya...
Cuba: Maandamano yafanyika Mara Mbili, Wengi Wakamatwa
Kikundi cha wanawake kijiitacho ‘wanawake wavaliao mavazi meupe’ (Ladies in White) kwa mara nyingine wametawala fikra za wanablogu wa Cuba waishio nje ya nchi. Maandamano ya amani ya kikundi hicho ambacho ni moja wapo ya vyombo vya upinzani vinavyoheshimika zaidi katika visiwa hivyo –pamoja na kukamatwa kwao mara kwa mara na vyombo vya dola –yanaendelea kuvuta hisia za watu. Mapambano ya hivi karibuni yalitokea mwishoni mwa juma lililopita wakati wanachama wa kikundi hicho walipojaribu kufanya maandamano mara mbili mjini Havana.