Habari kuhusu Sheria kutoka Januari, 2010
Naijeria: Uzoma Okere ashinda kesi dhidi ya jeshi
Nigerian curiosity anaandika kuhusu kesi ya Uzoma Okere huko Naijeria: “Uzoma Okere ni msichana wa Kinaijeria ambaye kipigo alichopata kutoka kwa maafisa wa jeshi kiliondokea kuwa video iliyosambazwa sana na...
Philippines: “Muswada wa Mkataba wa Ndoa Jadidifu”
Kikundi kimoja cha masuala maalum ya jamii nchini Philippines kinataka kuwasilisha sheria ambayo itaufanya mkataba wa ndoa kuwa na nguvu kwa miaka kumi tu. Pendekezo hilo la kipekee limezua mjadala mkali kwenye ulimwengu wa blogu.
Msumbiji: Kifo Cha Mradi Mkubwa wa Mazao Nishati
Mwishoni mwa mwezi Disemba, Baraza la Mawaziri la Msumbiji lilitoa tamko muhimu. Kibali cha kutumia Hekta 30,000 za ardhi kwa kampuni ya mazao nishati (biofuels) Procana, kimebatilishwa. Shauri la Mradi wa Procana, ulipo kwenye eneo kubwa linalopakana na Mbuga ya Taifa ya Limpopo ambayo imetanda mpaka nje mpaka wa nchi, lilikuwa na utata pamoja na mvutano mkubwa tangu (shauri hilo) lilipoanza mwanzoni mwa mwaka 2007.
Ethiopia: Adhabu ya Kifo Ili Kuwatisha Waethiopia
Berhanu Nega, mmoja kati ya watu waliohukumiwa kifo na mahakama ya Ethiopia anasema hashangazwi na adhabu ya kifo.
China: Adhabu ya Kifo kwa Akmal, ni Tendo la Kufuta Aibu ya Zamani
Akmal Shaikh, raia wa Uingereza aliyeshtakiwa kwa kuingiza mihadarati kinyume cha sheria nchini China, aliuwawa siku ya Jumanne japokuwa familia yake pamoja na serikali ya Uingereza waliomba adhabu ipunguzwe, wakidai...