Habari kuhusu Lugha

Maneno Yasiyotafsirika Yafafanuliwa kwa Michoro

  1 Juni 2014

Tovuti ya Pijamasurf [es] inazungumzia “orodha ya maneno 30 yasiyotafsirika” ambayo msanii mchunguzi Anjana Iyer [en] alijaribu kuyachorea mchoro wenye kuchekesha kidogo. Kwa mfano: Bakku- shan (Kijapani) Msichana mzuri…almuradi tu anaangaliwa kutokea nyuma. Unaweza kuipata orodha hiyo hapa.

Maandamano ya Taiwan ya #KupingaBunge, Yatafsiriwa

  21 Machi 2014

Mamia ya watafsiri wamejipanga kupitia mtandao wa facebook kutafsiri habari kuhusu maandamano ya raia wanaojikusanya kwenye Bunge la nchi hiyo kupinga hatua ya chama tawala nchini humo kupitisha mkataba wa kibiashara wenye utata na nchi ya China.

Honduras Yazindua Kamusi ya Mtandaoni ya Lugha za Asili

  28 Februari 2014

Kamusi ya lugha za asili nchini Honduras ilisambazwa mtandaoni hivi karibuni[es]. Gazeti la Honduras liitwalo Tiempo [es] linaeleza kuwa kamusi hii “imejumuisha maneno yanayofanana katika lugha ya Kihispaniola, chortí, garífuna, isleño, miskito, pech, tawahka na tolupán, lugha ambazo ndizo zinazotengeneza urithi wa lugha wa nchi hiyo.”  Kwa mfano, unapotafuta neno...

Wikipedia kwa Lugha ya Ki-Guarani

  2 Novemba 2013

Mwaka huu, Wikipedia katika lugha ya Kihispaniola ilifikia makala milioni moja na kutolewa kwa mwongozo msingi wa mtumiaji katika lugha ya ki-Guarani. Wazo ni kufufua jamii ya wanaozungumza kiguarani katika jukwaa hili kubwa. Hadi sasa kuna makala 20 tu katika lugha hiyo. […] Kama una nia ya kushirikiana na mradi...