Habari kuhusu Mawazo

Sababu za Kusafiri Mara Moja Moja

  29 Julai 2014

Kwenye blogu yake iitwayo Historias de una mujer lobo (Hadithi ya mbwamwitu wa kike), Natalia Cartolini anatafakari kuhusu sababu za kwa nini kusafiri kunaweza kuwa na faida kama, kwa maoni yake, “kutembelea maeneo mapya au kukutana na watu wapya wenye mtazamo mwingine ni muhimu wakati wote. Haijalishi kama unatoka kutembea...

Maneno Yasiyotafsirika Yafafanuliwa kwa Michoro

  1 Juni 2014

Tovuti ya Pijamasurf [es] inazungumzia “orodha ya maneno 30 yasiyotafsirika” ambayo msanii mchunguzi Anjana Iyer [en] alijaribu kuyachorea mchoro wenye kuchekesha kidogo. Kwa mfano: Bakku- shan (Kijapani) Msichana mzuri…almuradi tu anaangaliwa kutokea nyuma. Unaweza kuipata orodha hiyo hapa.

Hedhi Sio Siri ya Aibu. Tuzungumzie Siku Zetu kwa Uwazi

  26 Aprili 2014

“Kwa nini wanawake hawapendi kuzungumzia hedhi?” anauliza Sourav Kumar Panda kwenye tovuti ya Youth Ki Awaaz na anaendelea kujadili/a> kuwa kwenye siku hizi na zama za leo, kuendelea kuifanya hedhi kuwa suala la kuficha haina maana -wakati umefika kwetu kuvunja kimya na kuacha woga wa mila za jamii zetu kuhusiana...

Uchaguzi Mkuu wa India 2014: Kampeni Kwenye Mitandao ya Kijamii

  8 Aprili 2014

Mitandao ya kijamii imekuwa ni sehemu ya ugunduzi na ubunifu. Milind Deora [Waziri wa Muungano na Mbunge wa Mumbai Kusini] anatamba kuwa mgombea wa kwanza kupatikana kwa wapiga kura wake kwenye mtandao wa WhatsApp na BBM, na huko anajadili mpango kazi wake ikiwa ni pamoja na shughuli zake na mipango...

Mazungumzo ya GV: Kipi Kinafuata Nchini Ukraine?

  7 Machi 2014

Kipi kinafuata kwenye vuguvugu la maaandamano ya Ukraine? Maandamano na umwagaji damu ulisababisha kung'oka kwa rais anayetuhumiwa kuwa fisadi. Lakini sasa, wakati Urusi ikijiandaa kijeshi na Crimea ikifikiria kujitenga, yapo maswali mengi yasiyoisha kuhusu mustakabali wa kisiasa nchini Ukraine pamoja na uhusiano wake na Umoja wa Ulaya.

“Si rahisi kuwa Mhindi” nchini Marekani

  3 Machi 2014

Ricey Wild, Mmarekani wa asili anayeblogu kwenye blogu ya Indian Country Today, anandika kuhusu kuuawa kwa mbwa mwitu kwenye jimbo la Minnesota, Marekani. […]Rafiki yangu mpenzi Melissa alikuja kunichukua mwezi uliopita kwenda kwenye mkutano wa kupinga uwindaji wa mbwa mwitu kwenye jimbo la Mennesota na kwingineko. Tulipanda kaskazini na kuungana...