Habari kuhusu Mwitikio wa Kihisani
Miezi Michache Baada ya Kupotea kwa MH370, Kuanguka kwa Ndege Nchini Ukraine Kwawashitua Raia wa Malasia
Mhudumu wa ndege wa Malaysia aelezea katika Instagram na Twita kuhusiana na watu wengi kupoteza maisha katika matukio ya ajali za ndege za Malaysia: "Katika kipindi cha miezi minne niliwapoteza marafiki zangu takribani 30."
Je, Tunaweza Kuwasaidia Wazee kwa Kuwakumbatia? Kampeni hii ya India Yasema ‘Ndio!’
Kampeni ya KUKUMBATIA inafanya kazi kuunganisha pengo ya umri kati ya vijana na wazee katika juhudi za kupunguza hali ya kuwatenga wazee nchini India.
Hadithi ya Wakimbizi wa Njaa kutoka Niger katika Algeria Mashariki
Katika wiki chache zilizopita, mamia ya wahamiaji mwa Jangwa la Sahara kutoka Mali au Niger wamehamia miji ya Algeria katika mpaka wa Mashariki. Liberté Algérie anasimulia hadithi ya wale ambao waliamua kuhama na kwa nini [fr] Les conditions de vie au hangar de la cité Bourroh sont inhumaines. A l’intérieur...
Simulizi la Kusikitisha la Ibrahim na Djouma wa Jamhuri ya Afrika ya Kati
Djouma na Amadou Moussa ni wazazi wa Ibrahim. Djouma na Ibahim ni wahanga wa shambulizi la kikatili lililofanywa na wanamgambo waaasi, tukio lililokatisha maisha ya ndugu watano wa damu katika Jamhuri ya Afrika ya Kati, karibu na mpaka wa Kameruni. Wanamgambo hao walikuja wakati Amadou Moussa akiwa mbali na nyumbani kwake....
Mazungumzo ya GV: Ukoaji wa Mafuriko Uliowezeshwa na Watu Nchini Serbia
Juma hili tunazungumza na marafiki waishio Serbia wanajihusisha na jitihada za ukoaji. Je, ni hatua zipi zinazochukuliwa na wananchi na serikali? Na kwa nini mitandao ya kijamii iko hatarini?
“Hatujaweka Mkazo vya Kutosha Kwenye Afya ya Vijana”
Ripoti ya hivi karibuni kutoka kwa Shirika la Afya Duniani (WHO) kuhusu afya ya vijana duniani inabainisha kwamba: Sababu kubwa za vifo vya vijana duniani ni ajali za barabarani, VVU?UKIMWI, na kujiua. Duniani kote, wastani wa vijana milioni 1.3 walipoteza maisha yao mwaka 2012. Ripoti inaongeza vile vile kuwa :...
Baada ya Miezi Sita, Waathirika wa Kimbunga Haiyan Waendelea Kudai Msaada na Haki
Miezi sita baada ya kimbunga kikubwa kuharibu mamiliaoni ya makazi katika eneo la katikati ya Ufilipino, wahanga wanaendelea kuomba misaada na kutendelewa haki. Kuna madai ya kukosekana kwa mpango wa kurejesha hali kuwa ya kawaida.
Ni “Udhaifu” wa Serikali, Yasema Ripoti ya Ajali ya Kivuko cha Korea Kusini
Zimetimu siku 14 tangu kivuko cha Sewol kizame na watu 205 wamethibitika kupoteza maisha. Wanasiasa wanatumia tukio hilo na habari zisizosahihi za vyombo vya habari kuchochea hasira miongoni mwa Wakorea Kusini.
Mlipuko wa Homa ya Ebola Waua Watu 59 Nchini Guinea
Mlipuko wa homa ya Ebola umeua watu wasiopungua 59 nchini Guinea na matukio kadhaa yanayohofiwa kuwa ya homa hiyo yamekaribia kwenye mjini mkuu Conakry hiyo ikimaanisha kuwa ugonjwa huo unaweza kuenea kwenye mji mkuu wa Guinea. Barbara Krief anatoa taarifa za hivi karibuni [fr]: Au moins huit agents de santé...