Habari kuhusu Harakati za Mtandaoni kutoka Disemba, 2009
Austria: Jinsi Nyenzo Za Habari Za Kijamii “Zinavyoviwashia Moto Vyuo Vikuu”
Je, ulijua kwamba katika wakati huu vyuo vikuu vingi kote Ulaya vinakaliwa na wanafunzi? Vuguvugu hili lote limeratibiwa kwa kutumia nyenzo za uanahabari wa kijamii katika mtandao.
Namibia: Nafasi ya Vyombo Vipya vya Habari kwa Uchaguzi wa 2009
Uchaguzi wa rais na bunge la taifa la Namibia ulifanyika tarehe 27 na 28 Novemba 2009. Vyama vya siasa na mashirika yasiyo ya kiserikali yalitumia nyenzo kadhaa za habari za kijamii kupiga kampeni, kufuatilia na kuripoti Uchaguzi.
Indonesia: Sarafu za Kudai Haki
Raia wa mtandaoni (Netizens) wamezindua kampeni ya kukusanya fedha zilizo katika muundo wa sarafu ili kumuunga mkono Prita Mulyasari, mama wa nyumbani raia wa Indonesia aliyeandika malalamiko yake mtandaoni dhidi ya hospitali iliyotoa huduma mbaya, na ambaye alipatikana na hatia na mahakama moja ya kosa la "kuchafua jina" la hospitali hiyo binafsi.