· Oktoba, 2013

Habari kuhusu Uandishi wa Habari za Kiraia kutoka Oktoba, 2013

Rafiki Yangu Anateswa kwa Ku-blogu

GV Utetezi  5 Oktoba 2013

Safy ni mtu wa kawaida aliyewahi kufanya kazi kama afisa wa Teknohama mpaka aliposhuhudia rafiki yake akipigwa risasi na polisi wa kutuliza ghasia wakati wa majuma ya mwanzo ya mapinduzi. Hakuweza kuendelea kuwa "mtu wa kawaida" baada ya tukio hilo.

Korea Kusini: Mwandishi Msafiri, Utamaduni Tofauti, na Jamii ya Wageni

  4 Oktoba 2013

John Bocskay, mwanablogu asiyeandika mara nyingi sana alifanya mahojiano na mwandishi wa utalii Rolf Potts aliyetumia miaka kadhaa kwenye jiji la pili kwa ukubwa nchini Korea Kusini, Pusan, anasema: Kila mtu niliyeonana naye katika vilabu vya wageni alidai kuwa mwandishi au msanii, lakini hungeweza kuona maandishi mengi au sanaa. Ilikuwa...

Kuwasaidia Waathirika wa Tetemeko la Balochistan

  4 Oktoba 2013

Zaidi ya watu 300,000 wameathirika kufuatia tetemeko la hivi karibuni katika wilaya sita za Jimbo la Balochistan nchini Pakistan. Kashif Aziz wa mtandao wa Chowrangi anatoa habari za namna ya kutoa msaada kwa waathirika wa tetemeko la Balochistan.

Madaktari 400 wa Cuba Waenda Brazil

  3 Oktoba 2013

Daudi Oliveira de Souza, daktari na profesa wa Taasisi ya Utafiti wa Hospitali ya Sirio-Libanés, alituma barua ya wazi kwa madaktari zaidi ya mia nne wa Cuba ambao hivi karibuni waliwasili nchini Brazil wanaoanzisha kundi la kwanza la jumla ya madaktari 400 ambao wanatarajiwa kuja nchi hii kabla ya Desemba mwaka huu....