· Septemba, 2014

Habari kuhusu Uandishi wa Habari za Kiraia kutoka Septemba, 2014

Serikali ya Marekani Yadai Takwimu za Shirika la Indymedia Athens

  24 Septemba 2014

Mnamo Septemba 5, Wizara ya Sheria ya Marekani iliitaka shirika linaloshughulika na masuala ya kuhifadhi tovuti iitwayo  May First kutoa taarifa za mmoja wa wateja wake, ambaye ni Kituo cha Ugiriki cha cha Uandishi Huru Athens, kinachofahamika kama Indymedia Athens. Likiwa limeanzishwa mwaka 2005, May First ni shirika lisilo la kibiashara linalojikita...

Kimbia! Waislamu Wanakuja!

The Bridge  23 Septemba 2014

Mtazamo wa vyombo vikuu vya habari mara nyingi unaonesha “Waislamu” wenye sura moja kubwa, ambayo haikosi kuwa na ghasia. Kwenye kichekesho hiki kisicho na maana yoyote, Mchekeshaji wa ki-Pakistani Sami Shah anakuletea makundi makuu ya “waislamu”.

Uchafu Kutoka Viwandani Waua Mamia ya Ndege wa Porini Nchini Mongolia

  23 Septemba 2014

Zaidi ya ndege wa majini 500 wameonekana wakiwa wamekufa katika eneo la maziwa nchini Mongolia tangu kuanza kwa majira ya kipindi cha joto kutokana na maji kuchafuliwa. Maji hayo machafu, kama ilivyotaarifiwa na wafugaji wa maeneo hayo, maji haya yaliyochanganyikana na taka sumu yalitoka katika eneo la viwanda. Annie Lee...

Ushiriki Mkubwa wa Umma katika Mafunzo ya Tetemeko la Ardhi Nchini Mexico

  22 Septemba 2014

Mnamo Septemba 19, 1985, kwenye maeneo ya kati, Kusini na Magharibi mwa Mexico, hususani kwenye Wilaya ya Shirikisho, yalikumbwa na tetemeko kubwa, linalosemekana kuwa baya zaidi katika historia ya Mexico inayojulikana. Wakikumbuka miaka 29 tangu tukio hilo litokee, Katibu wa Ulinzi wa raia wa Wilaya ya Shirikisho aliandaa mafunzo ya...

Maktaba ya Digitali ya Tiba Asilia Nchini Ufilipino

  22 Septemba 2014

Ikiwa imeanzishwa na mamlaka kadhaa za kiserikali, Maktaba Dijitali ya Elimu ya Tiba za Jadi Ufilipino (TKDL-Health) inalenga kuweka kumbukumbu na kufanya masuala ya tiba za jadi kuwa za kidijitali nchini humo. Jamii, ambazo nyingi ni zile za miliamni au majirani zao, zimekuwa zikitegemea miti na mazao mengine ya asili...