Habari kuhusu Uandishi wa Habari za Kiraia kutoka Aprili, 2014
Win Tin: Mfungwa wa Kisiasa wa Myanmar Aliyefungwa kwa Muda Mrefu Zaidi Afariki Dunia
Mwandishi wa habari na mwanaharakati Win Tin ni mmoja wa viongozi wa harakati za kutetea demokrasia.
Magonjwa ya Afya ya Akili Hayapewi Kipaumbele Nchini Cambodia
Akiandika kwa niaba ya Southeast Asia Globe, Denise Hruby aliripoti jinsi wagonjwa wa akili katika maeneo mengi ya vijijini vya Cambodia wanavyofanyiwa: …Wagonjwa wa akili bado hutibiwa na waganga wa jadi, ambao lengo lao ni kuwatoa pepo wabaya kwa kuchoma ngozi, au kwa wafanyakazi wasio na ujuzi wa chumba kimoja...
Nukuu 8 za Kushangaza Zilizopata Kutolewa na Wanasiasa wa Malaysia
Balik Cina ni tovuti mpya ya habari inayokusanya nukuu za kuchekesha na za ajabu zinazotolewa na wanasiasa wa Malaysia.
Waziri Mkuu wa Zamani wa Malayasia Aitaka Boeing Kuwajibika kwa Ajali ya Ndege MH370
Waziri Mkuu wa zamani wa Malaysia Mahathir Mohamad ameitaka Boeing kuwajibika kufuatia tukio la kupotea kwa ndege ya Shirika la ndege la Malaysia yenye namba MH370. Hivi ndivyo alivyoandika kwenye blogu yake: Boeing ndiyo imetengeneza ndege hii. Boeing lazima waeleze inakuwaje njia zote za kuifuatilia mwenendo wa ndege hiyo ziweze...
Msiyalaumu Mataifa ya Magharibi kwa Matatizo ya Afrika
Gershom Ndhlovu anasema kuwa viongozi wa Afrika wanafanya kosa kuzilaumu nchi za Magharibi kwa matatizo ya Afrika: Kwenye mkutano wa hivi karibuni wa Umoja wa Ulaya ulifanyika nchini Ubeligiji, rais wa Zambia Michael Chilufya Sata alijibu mapigo kwa kile kile ambacho viongozi wengine wa Afrika walikisema huko nyuma kuhusu Nchi...
Hedhi Sio Siri ya Aibu. Tuzungumzie Siku Zetu kwa Uwazi
“Kwa nini wanawake hawapendi kuzungumzia hedhi?” anauliza Sourav Kumar Panda kwenye tovuti ya Youth Ki Awaaz na anaendelea kujadili/a> kuwa kwenye siku hizi na zama za leo, kuendelea kuifanya hedhi kuwa suala la kuficha haina maana -wakati umefika kwetu kuvunja kimya na kuacha woga wa mila za jamii zetu kuhusiana...
Kampeni ya ‘Piga Kura ya Hapana’ Yawahamasisha Waafrika Kusini Kuvitelekeza Vyama Vikubwa
Kikundi cha wanasiasa kimezindua kampeni ya "Amka! Tumechoshwa! mnamo April 15, 2014 wakati uchaguzi wa nchi hiyo umekaribia.
Maelfu Wamiminika Kumwona Yesu ‘Aliyetokea’ Nchini Cameroon
"Bado ninasubiri mtu aweke posti yenye picha aliyopiga na Yesu aliyetokea Odza."
VIDEO: Wanafunzi wa Iran Wavuruga Hotuba ya Mgombea Urais wa Chama Tawala
Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Amirkabir kilichopo mjini Tehran, nchini Iran waliimba nyimbo zenye vibwagizo vinavyomwuunga mkono Mir Hussein Mousavi na Mehdi Karroubi, ambao ni viongozi wa vyama vya Upinzani nchini humo waliowahi kuongoza maandamano ya Green Movement.
Mazungumzo ya GV: Moja kwa Moja kutoka Kombe la Dunia la Mtandaoni
Je, tuna mpango wa utawala wa mtandao wa intaneti duniani? Mazungumzo ya wiki hii yanakujia kutoka kwenye mkutano wa Net Mundial jijini São Paulo, Brazil.