Habari kuhusu Uandishi wa Habari za Kiraia kutoka Aprili, 2012
Indonesia: Maandamano ya Kupinga Bei ya Mafuta Yatikisha Majiji
Miji kadhaa ya nchini Indonesia iligubikwa na maandamano na vurugu za kupinga ongezeko la bei ya mafuta ya petroli katika wiki chache zilizopita. Wanahabari za mtandaoni walijadiliana ikiwa ongezeko hilo la bei lilikuwa jambo sahihi. Watumiaji wa Twita waliongeza nguvu ya wavuti wa kublogu ili kurusha taarifa za mapambano kati ya polisi na wanafunzi jijini Jakarta.
Zambia: Rais Awakera Raia Waishio Nje
Rais wa Zambia, Michael Sata, amewakasirisha raia wa nchi hiyo wanaoishi ng'ambo baada ya kuwakejeli wakati wa ziara yake ya siku tatu nchini Botswana na kufifisha matumaini yao ya kuanzishwa kwa uraia wa nchi mbili katika Katiba ya nchi ya hiyo.
Mali: Raia Washtushwa na Mapinduzi ya Kijeshi
Askari walioasi wametangaza kwamba wanatwaa madaraka nchini Mali, baada ya kuwa wameteka nyara kituo cha televisheni ya taifa pamoja na ikulu. Wanadai kwamba serikali ilishindwa kuvipa vikosi vya jeshi la nchi hiyo msaada ili kuwakabili vilivyo wapiganaji wa kabila la Tuareg waliokuwa wakiteka miji ya kaskazini mwa nchi hiyo.
Tanzania: Mwigizaji Nyota wa Filamu, Steven Kanumba, Afariki Dunia
Tanzania ilimuaga mmoja wa wasanii wake maarufu na nyota wa tasnia ya filamu, Steven Kanumba, kwa maziko yaliyogubikwa na majonzi mazito mnamo tarehe 11 Aprili 2012. Alifariki alfajiri ya Jumamosi, akiwa na umri wa miaka 28, baada ya kile kilichodaiwa kuwa ugomvi wa kimapenzi na rafiki yake wa kike aitwaye Elizabeth Michael kwa jina maarufu “Lulu”.
Malawi: Maoni ya Mtandaoni Kuhusu Kifo cha Mutharika
Victor Kaonga anaangalia maoni ya mtandaoni kufuatia habari za kifo cha Bingu wa Mutharika. Mutharika alikuwa rais wa tatu wa Malawi. Alifariki baada ya mshtuko wa moyo asubuhi ya Alhamisi. Hii ni mara ya kwanza kwa Malawi kumzika rais aliyefariki akiwa madarakani.
Taiwan: Kufukuzwa kwenye nyumba kwa nguvu kwa familia kwaitia dosari Sheria ya Ufufuaji Miji
Kufukuzwa kwa kinyama kwa familia ya Wang kulikotekelezwa na serikali ya Jiji la Taipei kulionyesha jinsi haki za raia zilivyo dhaifu mbele ya miradi ya ufufuaji mji. Kumekuwepo na maoni mengi yanayotaka Sheria ya Ufufuaji Miji irekebishwe.
Congo (DRC): Video zasaidia kumtia hatiani Thomas Lubanga kwa uhalifu wa kivita
Mnamo tarehe 14, Machi, mahakama ya kimataifa ya makosa ya kivita ilimtia hatiani Thomas Lubanga, kiongozi wa zamani wa waasi Kongo (DRC) Mashariki, kwa kosa la kuwatumia watoto katika vita. Jaji alisema picha za video zilizoonyesha mahojiano na askari hao watoto ziliziongeza uzito wa ushahidi ulioisaidia mahakama kutoa hukumu.
Ukraine: Gereza la Lukyanivska – “Mahali Watu Wanapotendewa kama Wanyama”
Mnamo tarehe 2 Aprili, Televisheni ya Ukraine ya TVi ilirusha filamu iliyotayarishwa na Kostiantyn Usov kuhusu hali ya maisha na jinsi mahabusu wanavyotendewa katika gereza la Kyiv la Lukyanivska, na pia kuhusu kuenea sana kwa rushwa miongoni mwa askari magereza. Kwa uchache, wengi katika wale ambao tayari wametazama video ya Usov walishtushwa sana na yale waliyoyaona.
Mexico: Mwaka mmoja tangu kuzaliwa kwa “Kundi la Harakati kwa ajili ya Amani, Haki na Utu”
Raia wa Mexico wanatoa maoni kuhusu kumbukumbu za mwaka mmoja tangu kuzaliwa kwa “Kundi la Harakati kwa ajili ya Amani, Haki, na Utu,” ambalo linahusiana na kifo cha mtoto wa mwanaharakati na mtunzi wa mashairi wa zamani Javier Sicilia wakati wa "vita" ambavyo utawala wa sasa umetangaza dhidi ya uhalifu wa kimtandao na kiimla.