Habari kuhusu Sauti Chipukizi

Tangazo la Shindano la Kupata Ufadhili wa Rising Voices 2014

Rising Voices inatangaza kuzindua shindano la ufadhili wa miradi ya kuwafikiwa watu kwa njia ya uandishi wa kiraia. Waombaji wanaweza kutuma mawazo yao kwenye tovuti na kupata mrejesho kutoka kwenye jamii zao wenyewe, kama namna ya kuboresha maombi yao na kushirikiana na wengine. Tarehe ya mwisho kutuma maombi ni Aprili 9, 2014.

14 Machi 2014

Simulia Hadithi Yako Kupitia Programu ya StoryMaker na Ushinde €1,000

Tumia Programu tumizi ya StoryMaker kusimuliza habari zako na ushindanie zawadi ya €1,000. Hadithi zote zitakazoingizwa kwenye www.storymaker.cc zinakuwa zimeingia kwenye mashindano. Shirika la Free Press Unlimited linatafuta hadithi bora ambayo ingebaki uvunguni bila kuwa na zana hiyo ya simu za mkononi mahususi kwa ajili ya kusimulia.

16 Novemba 2013

Paraguai: Kutoka Kutumikishwa Hadi Kuwa Kiongozi Mzawa.

Kutana na Margarita Mbywangi, ambaye katika umri wa miaka mitano, alichukuliwa kutoka kwa wazazi wake na kuuzwa mara kadhaa na kulazimishwa kufanya kazi za nyumbani. Tangu wakati huo amekuwa kiongozi muhimu wa kabila la Aché na hata kuwa Waziri katika nchi yake. Mbywangi sasa anasimulia maisha yake binafsi kupitia Mradi wa Rising Voices.

21 Julai 2012