Habari kuhusu GV Utetezi
Machapisho Katika Kurasa za Facebook Zachochea Ongezeko la Watu Kukamatwa Huko Bangladesh, Wavuti Waingiwa na Wasiwasi
Watu wawili walikamatwa Mei 14 na 15, kwa sababu ya maoni waliyobandika Facebook. Kukamatwa kwao kumeamsha hasira na wasiwasi katika mitandao ya kijamii huko Bangladesh.
Waandishi Wa Habari wa Msumbiji Waachiwa Huru Baada ya Kukaa Kizuizini Kwa Miezi Kadhaa Bila Kufunguliwa Mashtaka
Amade Abubacar na Germano Adriano walikuwa kizuizini tangu Januari lakini walishtakiwa tu hapo Aprili 16. Kwa sasa wanasubiri shauri lao lisikilizwe wakiwa chini ya uangalizi.
Waandishi wa habari wanawake nchini Uganda wanabeba ‘mzigo maradufu’ kutokana na mashambulizi ya mtandaoni pamoja na udhalilishaji
Waandishi wa habari wanawake nchini Uganda wanaubeba mzigo maradufu wa dhuluma inayotokana na jinsia mtandaoni ikiwa ni pamoja na vitisho vinavyohusiana na kuripoti taarifa za kisiasa. Vitisho hivi vinavyoendelea vimesababisha waandishi wa habari wanawake kujiondoa kwenye nyuga za umma.
Serikali ya Zimbabwe yaendelea kutumia habari za mtandaoni kama silaha ya kukandamiza haki za raia
Serikali mpya, iliyoongozwa na Emmerson Dambudzo Mnangagwa,iling’amua mara nguvu ya mitandao ya kijamii. Kama waziri wa zamani wa usalama wa nchi, Mnangagwa pia alitambua umuhimu na nafasi ya upotoshaji taarifa katika nyanja za kisiasa za Zimbabwe.
Je, Uganda itazima intaneti kadiri upinzani unavyozidi kuwasha moto kuelekea uchaguzi mkuu wa 2021?
Wakati uchaguzi wa 2021 unapokaribia, kuna uwezekano mkubwa kuwa utawala wa Uganda utaendeleza ukandamizaji wa wapinzani, ikiwa ni pamoja na kufunga mitandao ya kijamii.
Mwandishi wa Habari Tanzania Atekwa na Kufunguliwa Mashtaka Yenye Utata
Mwandishi Erick Kabendera ameandika kukoa ukandamizaji unaoendelea kuotoa mizizi chini ya Rais wa Tanzania John Magufuli. Jana, serikali ilimhukumu kwa makosa ya kiuchumi, lakini wakosoaji wanasema 'jinai kubwa aliyoifanya ni kuwa mwandishi wa habari.
Benin Yashuhudia Kuzimwa kwa Mtandao Siku ya Uchaguzi
Mtandao kufungwa ambapo ulifunguliwa usiku, ukiwaacha wapiga kura gizani siku ya uchaguzi.
Mfanyabiashara wa Slovakia Ashtakiwa kwa Kuamuru Mwanahabari Ján Kuciak na Mchumba Wake Wauawe
"Hii ni hatua kubwa muhimu, na ni nadra kuchukuliwa mwandishi wa habari anapouawa. Tunatarajia kuwa mamlaka zitatekeleza ahadi ya kuhakikisha haki inatendeka dhidi ya wote waliohusika."
Bloga wa Ki-Mauritania Akwepa Adhabu ya Kifo, Lakini Amebaki Kifungoni
Ould Mkhaitir alishtakiwa kwa kuandika makala iliyokuwa ikiikosoa wajibu wa dini katika mfumo wa kidini wa Mauritania.
Huru Mchana, Usiku Kifungoni: Mwanaharakati wa Kimisri Azungumzia Masharti ya Kufunguliwa Kwake
Wanaharakati, walioachiliwa hivi karibuni kutoka gerezani, uhuru wao kwa sasa unaanzia saa 12 asubuhi mpaka saa 12 jioni.