Habari kuhusu GV Utetezi kutoka Oktoba, 2015
Kampeni ya ‘Alaa Aachiwe’ Yashika Kasi Mwaka Mmoja Baada ya Kufungwa Kwake
Alaa Abd El Fattah ametumikia mwaka mmoja kwa sababu ya uanaharakati wake. Amebakisha miaka minne. Watumiaji wa mitandao wanapiga kelele wanapoadhimisha mwaka mmoja wa kifungo chake wakidai aachiliwe huru.
Wasiwasi wa Usalama wa Mfungwa wa Syria, Aliyehamishwa Kwenda Kusikojulikana
Wanaharakati wanaitaka serikali ya Syria kumwachia huru mara moja mwanablogu mfungwa mwenye asili ya Syria na Palestina Bassel Khartabil (Safadi) baada ya kuhamishwa mapema leo kutoka kwenye gereza alilokuwepo kwenda kusikojulikana.
Raia wa Ufaransa Wastukia Hatari ya Muswada wa Udukuzi
Watetezi wa haki za kiraia wanasema muswada unaokaribia kuwa sheria unaweza kuipa nguvu Ufaransa katika udukuzi wa kimataifa wa mawasiliano ya intaneti.