· Aprili, 2015

Below are posts about citizen media in Spanish. Don't miss Global Voices en Español, where Global Voices posts are translated into Spanish! Read about our Lingua project to learn more about how Global Voices content is being translated into other languages.

Habari kuhusu Kihispania kutoka Aprili, 2015

Je, Blogu Zinaelekea Kutoweka?

  25 Aprili 2015

Makala haya ni sehemu ya 46 ya #LunesDeBlogsGV (#JumatatuYaBloguGlobalVoices) siku ya Machi 23, 2015. Kwenye #LunesDeBlogsGV (#JumatatuyaBloguGlobalVoices), tunajitahidi kuzitunza blogu mithili ya “viumbe wanaoelekea kutoweka”, kwa kushughulikia changamto zinazokabili uwepo wa blogu kwenye ulimwengu wa kidijitali. Jitihada kama hizi zinamfanya mwanablogu Iván Lasso kuchambua mustakabali wa kublogu na matatizo yanayowakabili wanablogu leo,...

Kulinda Taarifa Binafsi Nchini Ajentina Bado Kuna Safari Ndefu

GV Utetezi  22 Aprili 2015

Kwenye makala iliyoandikwa kwa ajili ya gazeti la mtandaoni Haki za Kidijitali: Amerika Kusini & Visiwa vya Caribbean, No.21, Mmwanasheria wa ki-Ajentina Valeria Milanés anaeleza kwamba hata kama Marekani ni kiranja wa dunia kwenye kuchakata taarifa (data), bado haina sheria ya kulinda taarifa za watu. Marekani pia inachukuliwa kama nchi yenye “kiwango...

Nini Tofauti ya Kusoma na Kuelimika?

  22 Aprili 2015

Pedro Muller anatafakari kuhusu matatizo yanayoukabili mfumo wa shule, taasisi anayosema ilimaanisha mazingira tofauti ya kihistoria. Kwa kusema hayo, anabainisha umuhimu wa dhana hizi mbili zinazofanana lakini zikimaanisha nyakati mbili tofauti: “Kusoma” na “kuelimika”: El educar se va más allá de memorizarse un par de nombres y olvidarlos al siguiente...

Umoja wa Ulaya Hautatoa Nafuu ya Kodi ya VAT kwa Vitabu ya Kidigitali

  20 Aprili 2015

Mnamo Machi 5, 2015, Mahakama ya Haki ya Umoja wa Ulaya ilitoa hukumu kwamba punguzo la kodi ya ongezeko la thamani (VAT) lililotolewa kwa vitabu vinavyochapishwa halitahusisha vitabu vya kidijitali, kwa kuzingatia kwamba kila kinachosambazwa au kutolewa kwa mfumo wa kieletroniki au kwa mtandao wa intaneti ni huduma. Amalia Lopez anahoji...

Mwizi Akamatwa, Aomba Msamaha na Kusamehewa

  19 Aprili 2015

Labda alidhani ingekuwa vyepesi kuiba shampoo mali ya mmiliki wa duka nchini Peru, lakini mambo yalimwendea mrama mwizi huyu. Mtu mmoja akiwa ameongozana na mwenzake waliingia kwenye duka lililoko kwenye jiji la Huancayo nchini Peru, wakisema walikuwa wanataka kununua pombe, na mmiliki alipokuwa amepumbazwa kidogo, jamaa walibeba boksi la shampoo....

Kuhusu habari zetu za Kihispania

es