Habari kuhusu Kihispania kutoka Julai, 2014
Honduras Yazalisha Ajira kwa Kuhamasisha Shughuli za Jamii
Rais wa Honduras Juan Orlando Hernandes amezindua mpango wa “Desarrollemos Honduras” (Tuiendeleze Honduras), na maofisa na jamii walishiriki katika tukio hilo. Hernandes alieleza kwamba kama nyumba imebomoka au sakafu yake ni ya udongo, matengenezo lazima yafanyike kwa kutumia sementi; au kuweka vipaumbele kulingana na mahitaji ya familia, na: Cambiar los...
Sababu za Kusafiri Mara Moja Moja
Kwenye blogu yake iitwayo Historias de una mujer lobo (Hadithi ya mbwamwitu wa kike), Natalia Cartolini anatafakari kuhusu sababu za kwa nini kusafiri kunaweza kuwa na faida kama, kwa maoni yake, “kutembelea maeneo mapya au kukutana na watu wapya wenye mtazamo mwingine ni muhimu wakati wote. Haijalishi kama unatoka kutembea...
Tafakuri Baada ya Kombe la Dunia la FIFA 2014 Nchini Brazili
Mwanafunzi wa Mexico Álvaro anablogu kuhusu hisia na maoni yake kuhusu Kombe la Dunia la FIFA 2014 nchini Brazil. Anatafakari kuhusu kufanya vibaya kwa timu za mataifa ya Mexico na Brazili, lakini anasaili kile anachokiita kushindwa kwa mkakati wa Rais wa Brazili Dilma Rouseff. Días antes del comienzo del mundial,...
Namna ya Kuwa Baba Mwema
Raia wa Panama Joel Silva Díaz anafafanua kile ambacho kinawashangaza watu wengi, hususani wanaume: namna ya kuwa baba mwema. Kwenye blogu yake anaeleza changamoto alizokutana nazo na baba yake mwenyewe na kuhusianisha na malengo yake kama baba: …Recuerdo que veía como un juego el buscar un tema de conversación, debido...
Dondoo 13 za Kulinda Taarifa zako Kwenye Kompyuta Zinazotumiwa na Watu Wengi
Kama uko mbioni kwenda kwenye mapumziko na unafikiri kuchukua kompyuta yako na kuiunganisha na mtandao wa intaneti wa Siwaya (Wi-Fi) au kutumia kompyuta ambazo zinapatikana kwenye hoteli au kwenye eneo lolote la umma, unahitaji kusoma makala hii yenye dondoo 13 za kulinda taarifa zako, kama ilivyochapishwa na Andrea kwenye blogu...
Ajentina Yaichapa Uholanzi, Kukutana na Ujerumani Kwenye Fainali za Kombe la Dunia
Ajentina ilitinga katika fainali za kombe la Dunia kwa mara ya mwisho mwaka 1990 na ikapoteza kwa Ujerumani Magharibi, na hiyo inaufanya mchezo wa Jumapili na Ujerumani kuwa historia inayojirudia baada ya miaka 24.
Ajentina Yafurahia Mpinzani Wake wa Jadi Brazil Kuchapwa Vibaya na Ujerumani
Bendi ya Jeshi Alto Peru Mounted Fanfare Band ilipiga wimbo wakati wa gwaride la Siku ya Uhuru kwa kuchanganya na mashairi yenye vijembe kwa watani wao Brazili kukumbuka walivyowachapa kwenye mashindano ya Kombe la Dunia mwaka 1990.
Mjadala Kuhusu Upatikanaji wa Mtandao wa Intaneti Wazidi Kushika Kasi Nchini Cuba
Raia wa nchini Cuba waendelea kudai kupunguzwa kwa gharama za mtandao wa intaneti pamoja na urahisi wa upatikanaji wake.