Habari kuhusu Kijerumani
Alama ya Utambulisho wa Kompyuta ya Serikali ya Urusi Yakamatwa Ikihariri Makala ya Wikipedia ya Ndege ya MH17
Alama kadhaa za utambulisho wa kompyuta (IP address) ndani ya serikali ya Urusi zimeendelea kufanya kazi kazi kwenye kamusi elezo ya Wikipedia, ambapo kompyuta ya Shirika la Upelelezi la Urusi, FSO, ilihariri makala ya Kijerumani kuhusu Ndege ya Shirika la Ndege la Malaysia MH17, ikibadili neno “wanaotaka kujitenga” kuwa “waasi.” Teknolojia ya...
Jifunze Namna ya Kulinda Mawasiliano Yako ya Barua Pepe kwa Dakika Zisizozidi 30
Ulinzi binafsi wa Barua pepe , ni mwongozo wa anayetaka kujifunza kulinda barua pepe zake kwa kutumia Mfuko wa Zana Huru (FSF), uliotolewa katika lugha sita mpya [kifaransa, kijerumani, kijapani, kirusi, kireno, kituruki] mnamo Juni 30, 2014. Matoleo katika lugha nyinginezo yako mbioni kutoka. Hata kama huna cha kuficha, kutumia zana hii kunalinda faragha ya watu unaowasiliana nao,...
Orodha ya Waliouawa Katika Maandamano ya Venezuela Yapatikana kwa Lugha Tano
Katika blogu ya Panfleto Negro [es], John Manuel Silva na Emiliana Duarte wanafuatilia orodha ya vifo vilivyotokea kufuatia maandamano yanayoendelea nchini Venezuela. Orodha hiyo -ambayo awali ilikuwa kwa lugha ya Kihispania-imetafsiriwa kwenda lugha ya Kiingereza, Kijerumani, Kiitaliano/a> na Kifaransa.
Utambulisho wa Jamii ndogo ya Balkan
Waandishi vijana kumi na watano kutoka katika nchi zipatazo sita tofauti wametengeneza mfululizo wa masimulizi binafsi kuhusu masuala ya namna jamii zenye watu wachache (kwa mapana yake) zinavyoweza kuwakilishwa kutoka Bosnia na Herzegovina, Kosovo, Serbia, na Macedonia. Habari zinapatikana katika lugha za Kiingereza, Kijerumani, na Kifaransa katika mwonekano wa tovuti...
Austria: Jinsi Nyenzo Za Habari Za Kijamii “Zinavyoviwashia Moto Vyuo Vikuu”
Je, ulijua kwamba katika wakati huu vyuo vikuu vingi kote Ulaya vinakaliwa na wanafunzi? Vuguvugu hili lote limeratibiwa kwa kutumia nyenzo za uanahabari wa kijamii katika mtandao.
Video: Dunia Yaadhimisha Kuanguka kwa Ukuta wa Berlini
Leo ni Kumbukumbu ya 20 ya kuanguka kwa Ukuta wa Berlini, kizingiti madhubuti cha kiusalama ambacho kiliwahi kuligawa jiji la Berlini katika pande mbili za Mashariki na Magharibi huko Ujerumani. Leo tunaonyesha baadhi ya picha za video zinazotoka pande mbalimbali za dunia zinazopandishwa ili kusherehekea siku hii na nini ukuta huo ulimaanisha siyo Ujerumani tu bali duniani kote.
Macho ya Kimataifa kwenye Uchaguzi wa Marekani
Kadiri uchaguzi wa Marekani unavyokaribia, ndivyo kadiri macho ya kimataifa yanavyozidi kuelekezwa katika sera za nje za taifa hilo na wagombea wake wakuu. Kazimiradi kama vile ile ya Collective Journalism inayofanywa na Current TV (Uandishi wa Habari wa Umma wa Current TV) na Global Voices' Voices Without Votes (Mradi wa Global Voices - Sauti Zisizo na Kura) zimechukua jukumu la kukusanya taarifa na kuzipa mtazamo wa kimataifa katika masuala ya ndani ya sehemu fulani tu ulimwenguni.