Habari kuhusu Kifaransa kutoka Oktoba, 2012
Ghana: Vikwazo Vinavyowakabili Wanawake Kimaendeleo
Betty Mould Iddrisu, Jaji na Waziri wa Sheria wa Ghana, anaandika [fr] kwenye blogu ya pambazuka.org: Kufikia ngazi za juu kabisa za utawala si rahisi, na hata unapopanda mpaka juu kabisa, bado unajikuta unakabiliwa na hisia za watu zenye uadui na watu wanakuwa na mashaka na uwezo wako, kwa sababu...
DRC Kongo: Misuguano Kati ya Kinshasa na Paris Mkutano Unapoanza
Le Potentiel anaandika kwamba [fr] tathmini ya Uvunjaji wa Haki za Binadamu nchini DRC Kongo iliyofanywa na Rais wa Ufaransa Hollande haikuchukuliwa kijuu juu na serikali ya Kongo wakati ambapo Mkutano wa nchi zizungumzazo Kifaransa ndio kwanza umeanza mjini Kinshasa, DRC. SErikali hizi mbili zinaonekana kutofautiana sana kuhusu mambo kama...
Côte d'Ivoire: Wafanyakazi wa Afya Wagoma baada Miezi Minne Bila Mshahara
S.B anatoa maoni juu ya kuanza kwa mgomo usio na ukomo unaoratibiwa na wafanyakazi wa taasisi za afya mjini Abidjan. Katika mtandao wa Connection Ivorienne, anabainisha [fr] kwamba: Kufuatia mabadiliko ya utolewaji wa huduma za afya ambazo zilitolewa bure kabisa baada tu ya kumalizika kwa mgogoro wa baada ya uchaguzi,...