Habari kuhusu Kifaransa kutoka Disemba, 2011
Dondoo za Video: Maandamano, Chaguzi, Utamaduni na GV
Baadhi ya habari za kuvutia za Global Voices na video za hivi karibuni kutoka Mashariki ya Kati na Afrika Kaskazini, Afrika kusini mwa Jangwa la Sahara, Mashariki na Ulaya Kati, Karibeani pamoja na Marekani ya Kusini, zimeletwa na Juliana Rincón Parra.
Kongo (DRC): Wakongo Waishio Nje ya Nchi Walipuka Kumpinga Kabila
Wakati Kongo (DRC) ikingoja matokeo ya mwisho ya kura za Urais na wabunge, wa-Kongo waishio nje ya nchi hiyo, ingawa hawakuruhusiwa kupiga kura, wameonyesha kujitolea kwako kwa kuzifanya sauti zao zisikike. Julie Owono anataarifu.
Madagaska: Wajadili Uhalali wa Uwekezaji wa Kigeni wa Moja kwa Moja
Wakati Madagaska ikijaribu kutafuta suluhisho la matatizo ya muda mrefu ya kiasa, Wanablogu wa ki-Malagasi wanajadili thamani ya Uwekezaji unaofanywa Moja kwa Moja na raia wa Kigeni. Wa-Malagarasi wanaamini kwamba Madagaska, kama nchi nyingine za Kiafrika inao utajiri mkubwa wa rasili mali lakini tatizo likiwa ardhi yenyewe kupokonywa kwa sababu ya utawala mbovu na biashara zisizoangalia maslahi ya wananchi.