Habari kuhusu Kibahasa
Miezi Michache Baada ya Kupotea kwa MH370, Kuanguka kwa Ndege Nchini Ukraine Kwawashitua Raia wa Malasia
Mhudumu wa ndege wa Malaysia aelezea katika Instagram na Twita kuhusiana na watu wengi kupoteza maisha katika matukio ya ajali za ndege za Malaysia: "Katika kipindi cha miezi minne niliwapoteza marafiki zangu takribani 30."
Italia Yalaumiwa kwa Ukiukaji wa Haki za Wakimbizi wa Kiafrika
Februari 23, Mahakama ya Haki za Binadamu ya Ulaya huko Strasbourg ilikuja na hukumu ya kihistoria kwamba Italia imevujna Tamko la Ulaya la Haki za Binadamu kwa kuwazuia na kuwarudisha wakimbizi wa ki-Eritrea na Somalia kwenda Libya. Abdoulaye Bah anaripoti.
Indonesia: Maandamano ya Kupinga Bei ya Mafuta Yatikisha Majiji
Miji kadhaa ya nchini Indonesia iligubikwa na maandamano na vurugu za kupinga ongezeko la bei ya mafuta ya petroli katika wiki chache zilizopita. Wanahabari za mtandaoni walijadiliana ikiwa ongezeko hilo la bei lilikuwa jambo sahihi. Watumiaji wa Twita waliongeza nguvu ya wavuti wa kublogu ili kurusha taarifa za mapambano kati ya polisi na wanafunzi jijini Jakarta.
Indonesia: Sarafu za Kudai Haki
Raia wa mtandaoni (Netizens) wamezindua kampeni ya kukusanya fedha zilizo katika muundo wa sarafu ili kumuunga mkono Prita Mulyasari, mama wa nyumbani raia wa Indonesia aliyeandika malalamiko yake mtandaoni dhidi ya hospitali iliyotoa huduma mbaya, na ambaye alipatikana na hatia na mahakama moja ya kosa la "kuchafua jina" la hospitali hiyo binafsi.
Indonesia: Tetemeko Kubwa Laikumba Sumatra
Mji wa mwambao wa Padang, Sumatra Magharibi umeharibiwa tena na tetemeko la ardhi.