makala mpya zaidi zilizoandikwa na Rose Kahendi kutoka Disemba, 2013
China: Mashindano ya “Akina Mama Wanaotamanisha”
Sina Weibo, tovuti ya Kichina inayofanana na Twitta, imeandaa mashindano ya “Akina Mama Wanaotamanisha.” Picha za washindani zinaonyesha wazi kwamba wengi wao sio akina mama halisi. Hata hivyo, hizo picha zinatuambia mengi kuhusu uhusiano wa kijinsia nchini China. Soma mengine kwenye tovuti ya Offbeat China.
Misri: Picha 27 kutoka Hala'ib
Mwanablogu Mmisri, Zeinobia, amesambaza onyesho hili la picha kutoka Hala'ib, bandari na mji katika mwambao wa Bahari ya Shamu, kwenye Pembetatu ya Hala'ib, karibu na mpaka wa Sudan: Tazama “yasiyoeleweka” kwenye Storify
Hali ya Uhuru wa Dini Nchini Maldivi
Maldivi ni miongoni mwa nchi za kwanza kwenye orodha ya serikali zinazozuia uhuru wa dini. Ni lazima raia Wamaldivi wawe Waislamu, na hawawezi kufuata dini yoyote isipokuwa Uislamu. Wageni wasio Waislamu hawawezi kupiga kura, kuabudu hadharani, kupata uraia, wala kutumikia umma. Kwa maoni ya Mwanahabari Hilath Rasheed, huenda nchi ya...
“Mimi ni Mchuuzi Mjerumani Mjini Dakar”
Muda mfupi baada ya kuwasili kwangu Senegal, nilikutana na kijana. Alinieleza hamu yake ya kuondoka Senegal katika mkutano wetu wa kwanza. Nilitaka kuelewa yaliyosababisha hamu yake ya kuondoka na hali ya maisha yake ya kila siku ili nipate kufahamu maelezo ya kijamii na ya kiutamaduni ya kutaka kwake kuondoka. Alikuwa...
Ulaya Yamuonya Waziri wa Ufaransa Kuhusu Matamshi Yake Dhidi ya Warumi
Matamshi ya Waziri wa Mambo ya Ndani wa Ufaransa, Manuel Valls, yalifufua uhasama uliokuwepo kati ya Ufaransa na Warumi.