makala mpya zaidi zilizoandikwa na j nambiza tungaraza kutoka Januari, 2010
Haiti: Ramani za Kwenye Mtandao Zaonyesha Uharibifu Pamoja na Jitihada za Kusambaza Misaada
Marc Herman anaziangalia kwa karibubaadhi ya ramani ambazo watoaji misaada wanazitumia ili kuwasilisha hali inayobadilika kila wakati katika maeneo ya tetemeko la ardhi nchini Haiti. Karibu ya juma moja baada ya janga kutokea - na matetemeko yaliyofuatia ambayo yalifanana na matetemeko mengine makuu – ramani na taswira za setilaiti zinajidhihirisha kuwa ni taarifa pekee ambazo zinaweza kutegemewa.
Senegal Yatoa Ardhi ya Bure kwa Walionusurika na Tetemeko la Ardhi
Rais wa Senegal, Abdoulaye Wade, ametawala vichwa vya habari kwa kutoa ardhi ya bure kwa Mu-Haiti yeyote aliyenusurika na tetemeko na ambaye “atapenda kurejea kwenye asili yake” kwa mujibu wa msemaji wake. Kwenye wavuti, tangazo hilo limepokelewa na watu wengi kwa kejeli.
Haiti: Twita Kutoka Eneo La Tukio
Wakati habari za tetemeko la ardhi huko Haiti zikitoa mwangwi duniani kote, wakazi majasiri, wanahabari wan je, na wafanyakazi wa misaada wanaandika jumbe za twita kutokea katika eneo lililoathirika. Baadhi yao wanafanya kazi ya kukusanya misaada na fedha, wakati wengine wanajaribu tu kuionyesha dunia mambo yanavyooendelea nchini Haiti.
Baada Ya Tetemeko la Ardhi, Jumbe za Twita Kutoka kwa Walioshuhudia
Kutokana na janga la tetemeko la ardhi lenye ukubwa wa 7.0 ambalo limekikumba kisiwa cha Haiti jioni ya leo (Januari 12), “Haiti” ni mada kuu hivi sasa kwenye huduma ya Twita. Miongoni mwa lundo la jumbe zinazotumwa tena na tena za taarifa za habari kutoka za vyombo vya habari vikubwa na jumbe nyingine za twita zinazotuma sala au dua pamoja na salamu za heri kwa kisiwa hiki cha Karibea, pia kumekuwepo taarifa za mashahidi waliopo kwenye tukio kama vile mwanamuziki na mwendesha hoteli Richard Morse, ambaye anatwiti kwa jina la @RAMHaiti.
Haiti: Maoni ya Mwanzo Kuhusu Tetemeko la Ardhi Lenye Ukubwa wa 7.0
Posti ya kwanza ya blogu iliyoandikwa kwa lugha ya Kifaransa kuhusu tetemeko la ardhi huko Haiti imetokea nje ya nchi hiyo, ikitangaza habari mbaya za kuanguka kwa Kasri ya Rais, hospitali na majengo mengine na pia tishio la tsunami. Kwa mujibu wa MetropoleHaiti, Marekani tayari imekwishapendekeza misaada ya kibinadamu.
China: Kwa Heri Google
Kufuatia tangazo la Google leo kuwa ikiwa serikali ya China haitaruhusu tawi lake la China kusitisha uzuiaji wa matokeo ya kutafuta tawi la Google nchini China litafungwa, wanamtandao walitembea mpaka kwenye ofisi za Google mjini Beijing ili kuweka maua. HABARI MPYA: picha zaidi hapa, uwekaji rasmi wa maua (ya rambirambi)...
Afrika: Matangazo ya “AdWords” Katika Afrika
Miquel anajadili matangazo ya Google AdWords katika Afrika: “Wakati ingelikuwa ni njia nzuri sana kwa wanablogu wa Kiafrika kupata pesa kidogo ili kulipia gharama za intaneti, Google haitoi chaguo la malipo kwa nchi yoyote ya Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara.”
Bolivia: Mshindi wa Zamani wa Mashindano ya Urembo Atangazwa Kugombea Ugavana wa Jimbo la Beni
Bolivia Jessica Jordan kuwa mgombea wa kiti cha ugavana kwa tiketi ya Chama Cha Ujamaa (MAS) huko kwenye jimbo la Beni, ambalo kwa kawaida hudhibitiwa na upinzani.
Misri: Mauaji ya Kinyama ya Naga Hammady
Wanablogu wa Misri wanaelezea kustuka kwao na hasira kwa kuuwawa kwa Wakristu wa dhehebu la Koptiki wakati wa mkesha wa sikukuu yao ya krismasi huko Naga hammady, katika Misri ya Juu. Mhalifu asiyejulikana alipiga risasi hovyo hovyo kwenye umati watu baada ya waumini kumaliza maombi na wakiwa wanaelekea majumbani kwao.
Angola: Kombe La Mataifa ya Afrika Moja Kwa Moja Kwenye Mtandao
Pata habari za Kombe la Mataifa ya Afrika yanayofanyika nchini Angola moja kwa moja: “Kwa wale ambao wangependa kuangalia Kombe la Mataifa ya Afrika 2010 kwenye mtandao, kutakuwa na tovuti za michezo zinazotoa mtiririko wa mapambano ya mpira moja kwa moja mtandaoni, bure.”