j nambiza tungaraza · Novemba, 2009

makala mpya zaidi zilizoandikwa na j nambiza tungaraza kutoka Novemba, 2009

Misri: Haki ya Kijerumani kwa Marwa El Sherbini

Muuaji wa Marwa El-Sherbini, mwanamke wa Kimisri ambaye alichomwa visu mpaka kufa na muhamiaji mwenye asili ya Urusi na Ujerumani, Alex Wiens, ndani ya mahakama huko Ujerumani, amehukumiwa kifungo cha maisha, bila uwezekano wa kuachiwa mapema. Haki hatimaye imetolewa na muuaji anaadhibiwa, wanasema wanablogu wa Misri.

India: Usawa

  15 Novemba 2009

“Takriban asilimia 15 ya watu ambao ni viongozi wa siasa na watumishi wa serikali, kwa kupitia vitendo vya kifisadi, wamejilimbikizia asilimia 85 ya utajiri wote wa India, na kuwaachia asilimia 15 tu ya utajiri huo asilimia 85 ya wananchi,” anasema Ram Bansal katika blogu ya India in Peril.

Algeria-Misri: Ugomvi Juu ya pambano la Mpira kwenye Mtandao

Hali tete kati ya mashabiki wa mpira wa miguu wa Misri na Algeria inazidi kukua kabla ya pambano litakalofanyika mjini Cairo tarehe 14 Novemba. Mchuano huo utaamua ipi kati ya timu hizo zitafaulu kwenda kwenye Kombe la Dunia la FIFA Afrika ya kusini mwaka ujao. Misri inahitaji japo ushindi wa magoli mawili ili kulazimisha mchezo wa kukata shauri katika uwanja wa nchi nyingine ambapo Algeria, ambayo imeshindwa kufaulu kwenda kombe la dunia tangu 1986, itapambana ili kutunza nafasi yake ya sasa ya kuongoza katika kundi la wanaogombania nafasi ya kufaulu. Wakati wa kuelekea pambano la Jumamosi, mashabiki washindani wamekuwa wakijiandaa nje ya mtandao wa intaneti, kadhalika katika malumbano makali ya mtandaoni, ambayo yamekua na kugeuka “vita-vya-mikwara-kwenye-mtandao”

Syria: Simulizi Ya Ufukweni

Profesa wa Fasihi ya Kiingereza kutoka mji wa mdogo wa Tartous huko Mediterranean na mwandishi mwenye asili mchanganyiko ya Siria na Canada wakiwa safarini kuelekea kwenye nchi yake ya asili wanatizamana wakiwa kwenye mgahawa unaoitwa Sea breeze. Hivyo ndivyo Mariya na Abu Fares walivyoamua kuanza shani yao na kuwanasa kwa wasomaji wao. Yazan Badran anatupasha.

Jordan: Barua kwa MBC

M-jordan Ola Eliwat, kutoka Cinnamon Zone, anaandika barua ya wazi kwa makapuni ya televisheni ya MBC. Katika barua hiyo anaandika: “Na tafadhali fikirieni kufunga 90% ya idhaa zenu, nadhani itakuwa hisani KUBWA kwa taifa la Kiarabu!”