makala mpya zaidi zilizoandikwa na j nambiza tungaraza
Kuwait: Nampenda Osama Bin Laden
Mwandishi wa makala wa Kuwait Khulood Al-Khamisametangaza mapenzi yake ya dhati kwa kiongozi wa ugaidi Osama Bin Laden, anasema kuwa anasubiri kuungana naye ahera ili aweze kutimiza ndoto yake. Kwenye Twita watu wa Kuwait wanaeleza kustushwa kwao na makala hiyo pamoja na hisia za moyoni za Al-Khamis.
Naijeria: Gavana wa Kinaijeria Kwenye Twita
Gavana wa Kinaijeria Kayode Fayemi yumo kwenye Twita, mwanablogu wa Naijeria Lord Banks anaripoti.
Uganda: Wananchi Wakasirishwa na Kukamatwa Kikatili kwa Kiongozi wa Upinzani
Kiongozi wa upinzani nchini Uganda Dk.Kiiza Besigye alikamatwa tena katika mji mkuu wa Kampala kutokana na kushiriki kwake katika Kampeni ya Kutembea Kwenda Kazini usiku mmoja baada ya kuachiwa huru kwa dhamana. Besigye alipewa dhamana kwa sharti kuwa asijihusishe na kampeni ambayo imeuweka utawala wa Uganda kwenye vichwa vya habari kwa majuma matatu sasa.
Msumbiji: Polisi Washambulia Waandamanaji
Siku ya tarehe 6 Aprili, maofisa wa tawi la Polisi wa jamhuri ya msumbiji (PRM) – Kikosi cha Askari Maalum wa Dharura (FIR) – walitumia nguvukusitisha maandamano ya wafanyakazi wa shirika binafsi la ulinzi Group Four Security (G4S). Kwenye Facebook, wanamtandao walionesha kuchukizwa kwao kutokana na vitendo hivyo vya kikatili na kuhoji wajibu wa polisi, sheria na haki za binadamu.
Kenya: Uanahabari wa kiraia wa Mtandao wa Habari wa Kibera
Vijana wa Kibera, Kenya, kitongoji ambacho kinajulikana kwa baadhi kama eneo kubwa la hovyo zaidi ya yote barani Afrika, wamedhamiria kuonesha sura nyingine ya mahali wanapoishi. Huku wakiwa na kamera mkononi, wanavinjari mitaa kutafuta habari kuinesha dunia jinsi Kibera inavyojiona yenyewe.
Naijeria Yapiga Kura 2011: Maoni kutoka kwenye Uchaguzi
Wanaijeria walipiga kura jana katika uchaguzi wa tatu wa rais tangu taifa hilo lilipoingia kwenye utawala wa kiraia mwaka 1999. Mpaka sasa, uchaguzi huo umeelezwa na wengi kuwa ulikuwa wa mafanikio, huku kukiwa na taarifa za ghasia za hapa na pale pamoja na hitilafu za upigaji kura. Vyanzo vya habari vimeripoti kuwa watu wengi walijitokeza, foleni zenye kufuata utaratibu, na wapiga kura kusubiri hadi uchaguzi utakapomalizika ili kuhakikisha kwamba kura zao zimehesabiwa. Wanablogu wanajadili.
Côte d'Ivoire: Kuanguka kwa Laurent Gbagbo
Laurent Gbagbo alikamatwa katika makazi yake ya Cocody, pamoja na mkewe, Simone, na msafara wa watu wa karibu. Miezi mitano baada ya kukataa kukabidhi madaraka kwa rais anayetambuliwa kimataifa kama rais mpya wa Côte d'Ivoire, Alassane Ouattara, mgogoro nchini humo hivi sasa unaelekea kufikia hitimisho.Mtiririko wa matukio yaliyopelekea kukamatwa kwa Gbagbo yaliorodheshwa kwa kina kwa njia ya video za kwenye mtandao ambazo zilitolewa maoni kwenye mtandao.
Naijeria: Maonesho ya Picha za Kampeni ya Urais
George Esiri alifuatilia kampeni za kugombea urais za chama cha PDP huko Naijeria. Maonesho ya picha alizopiga yalizinduliwa jana katika Kituo cha Yar'Adua.
Côte d'Ivoire: Televisheni ya Taifa RTI Inawezekana kuwa Inatangaza Kutokea Kwenye Gari la Matangazo
Kama vile alivyoelezea Julie Owono , ni vigumu kupembua mapambano ya kudhibiti vyombo vya habari vya Pwani ya Pembe (Cote d'Ivoire). Taarifa kutoka Waandishi Wasio na Mipaka inaashiria kuwa RTI inaweza ikawa inatangaza kutokea kwenye gari lililoegeshwa kwenye nyumba ya mtu binafsi (fr).
Gabon: Wanafunzi Waandamana, Wanajeshi Wasambazwa
Mgogoro wa kisiasa nchini Gabon ulifikia vilele vipya siku ya Alhamisi, wakati wanafunzi walipoandamana katika Chuo Kikuuu cha Omar Bongo kilichopo ndani ya mji mkuu wa nchi hiyo, Libreville. Wakati maandamano ya juma lililopita yalishirikisha zaidi wanachama wa vyama vya upinzani, mgogoro huu unaonekana kupelekea kuwa mgogoro mkubwa zaidi wa kijamii.