makala mpya zaidi zilizoandikwa na Eric Nyagah
Baada ya Kony 2012, “What I Love About Africa” Yanyakua Mazungumzo
Kampeni katika mtandao kuhusu mhalifu wa kivita Joseph Kony umesababisha utata mkubwa barani Afrika. Kampeni nyingine ya kupinga utata huo na kuonyesha upande bora wa bara la Afrika, unaojulikana kama #WhatILoveAboutAfrica (Nini Ninachopenda Kuhusu Afrika) sasa unaenea katika tovuti la Twitter.
Colombia: Mwanahabari Raia Atishwa Kuhusu Video Iliyoenea
Mwanahabari raia Bladimir Sánchez ameshapata vitisho kwa maisha yake kwa kueneza video inayoonhesha kuhamishwa kwa fujo kwa wakulima na wavuvi wanaopinga ujenzi wa bwawa la kuzalisha umeme katika eneo la Huila, nchini Colombia. Baada ya muda usiozidi siku tatu, watu zaidi ya 600,000 wameitazama.
Habari za Ulimwengu: Mikesha ya Mshikamano na Wanatibeti
Tangu mwezi Februari 2009, WaTibeti 23 wamejichoma moto ili kudai Tibeti huru na kurejea kwa Dalai Lama. Katika mwezi wa mwaka mpya wa kiTibeti, wanaharakati kutoka duniani kote wanaonyesha jinsi wanavyowaunga mkono waTibeti kwa maandamano na dua.